Header AD

Aliyeng’atwa ulimi kushtakiwa


Majeruhi wa kung’atwa ulimi, Saidi Mnyambi (26),  amefunguliwa shtaka la kujaribu kubaka.
Mnyambi ambaye aling’atwa ulimi hadi kukatika na mwanamke kwenye tukio la ngono, ‘kibao’ kimemgeukia na yuko chini ya ulinzi wa polisi wodi namba nne alikolazwa kwa takriban wiki moja akituhumiwa kwa jaribio la ubakaji.

Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba amesema wanamshikilia Mnyambi baada ya awali kumkamata Mwajabu Jumanne (36) kwa tuhuma za kujeruhi kwa kung’ata ulimi.

“Tumelazimika kuwashikilia wote wawili kutokana na kila mmoja kumtuhumu mwenzake. Baada ya uchunguzi wa kina tutafikia maamuzi stahiki,” amesema.
Aliyeng’atwa ulimi kushtakiwa Aliyeng’atwa ulimi kushtakiwa Reviewed by Unknown on Septemba 21, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads