KHALFANI-: SIJAONA DIRECTOR WA KUNINYIMA USINGIZI HAPA BONGO
Ikiwa tasnia inazidi kukua siku hadi siku na mabadiliko makubwa katika game ya Bongo Fleva kuzidi kuonekana ikiwa ni kuanzia kwenye utengenezaji wa audio mpaka video
na kupelekea ushindani mkubwa katika game.
Director Khalfani amefunguka kuwa haoni ushindani katika soko la madirector wa sasa hapa Bongo na hivyo hakuna director wa kumnyima usingizi.
Akiongea na Perfect255 Khalfani amedai kuwa madirector wa Bongo hawana ubunifu, bali kila siku wanarudia vitu vile vile ambavyo vinafanyika kila siku.
“Madirector wapo wengi sana hapa Tanzania lakini hawafanyi kazi nzuri. Mara nyingi huwa nalaumu sana kwasababu hawatupi chalenges madirector wa Bongo. Kila siku video ni zile zile, wanashoot mbele ya magari, kwenye ma-sweeming pool, nyumba kali, kwahiyo hakuna ubunifu.”
KHALFANI-: SIJAONA DIRECTOR WA KUNINYIMA USINGIZI HAPA BONGO
Reviewed by Unknown
on
Januari 24, 2017
Rating:
Post a Comment