STORY:MJUKUU WA MSUKULE PART(20)
MAIFO93.BLOGSPOT.COM
STORY:MJUKUU WA MSUKULE
PART(20)
MWANDISHI:Amani Zabranco
STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART 20)
STORY:MJUKUU WA MSUKULE
PART(20)
MWANDISHI:Amani Zabranco
Mara akaingia yule kikongwe akiwa na wale walinzi, akasema anataka kuondoka na Saguda, Saguda akamuomba yule kikongwe kua atoke pamoja na yule rafiki yake aliyempata mule ndani ya chumba cha misukule. Yule bibi akamkubalia na wote wawili wakatoka kuelekea kwenye jengo la Yule kikongwe.
Walipofika mule ndani yule kikongwe akamuuliza Saguda kama amekula, lakini Saguda akajibu kuwa hajala chochote, Yule bibi akamletea chakula
kizuri cha kawaida kisha Saguda akala hadi akatosheka.
kizuri cha kawaida kisha Saguda akala hadi akatosheka.
Miezi nane ikapita huku kila mbinu aliyokuwa anaipanga Saguda kwa ajiri ya kutoroka ikawa inashindikana, siku moja yule bibi akawaita saguda na rafiki yake yaani yule msukule aliyejuana naye pale gamboshi. Kisha kikongwe akawapa ramani nzima ya kutoroka pale gamboshi. Akawaambia kwamba, ‘’kwanza inabidi mkatafute kibuyu ambacho kipo kwenye pango kubwa ambalo lipo ndani ya h ii himaya, hicho kibuyu ndiyo kina dawa ambayo mtu akijipaka wachawi wala mizimu haiwezi kumuona’’.
Yule bibi akaendelea kuwapa ramani nzima, akawa anawaambia kuwa ndani ya pango ambapo ndipo kuna hivyo vibuyu, kuna nyoka mkubwa wa ajabu na mkali ambaye anavilinda hivyo vibuyu. Saguda aliposikia vile akaanza kuwaza jinsi kazi ya kutoroka itakavyokuwa ngumu, yule rafiki yake na Saguda akakubali hata kufa ili Saguda afanikishe kuipata ile dawa.
Kikongwe akatoa hirizi nyeusi akampa Saguda akamuambia kuwa itawasaidia ili mizimu isiwadhuru wanapoingia kwenye lile pango. Lakini yule kikongwe akawaambia kuwa wakikamatwa wasimtaje kwa kua ataonekana ni msaliti ndani ya ile himaya.
Mara Sauti za ngoma zikasikika kwa nje, yule bibi akasema ‘’leo ni siku ya kula nyama ya mtu kuna watu wa kutolewa kafara wameletwa, kwa hiyo gamboshi nzima inasherekea kwa kula nyama zao!!!’’. Saguda naye akawa na hofu kuwa huenda akala nyama ya mtu, saguda akaamua kumuuliza yule bibi ‘’bibi hivi hata mimi watanilazimisha kula nyama ya binadamu????’’. Yule kikongwe akasema kuwa sheria ni lazima watu wote pale gamboshi washiriki kwenye hiyo sherehe ikiwa ni pamoja na kula nyama za watu.Firimbi na ngoma zikazidi kutawala kwa kule nje, yule bibi akamuambia saguda kuwa inabidi waende chini ya mti wa mbuyu ambapo ndipo ngoma zinapigwa, lakini kikongwe akamuambia yule rafiki yake na saguda aondoke na arudi kwenye kile chumba cha misukule, kwa kuwa misukule hawaruhusiwi kujichanganya na watu wengine.
Yule bibi akasema inabidi kwanza ampeleke saguda jikoni ili akaone mapishi ya gamboshi jinsi yalivyo. Wakaondoka na Saguda kuelekea jikoni kwa kuwa yule bibi alikuwa ni mkuu wa kitengo cha mapishi pale gamboshi, walipofika jikoni Saguda hakuamini macho yake kuona masufuria makubwa yakiwa yamejaa vipande vya nyama za watu. Saguda akazidi ku……………….(USIKOE SEHEMU INAYOFUATA @ mainfo93.blogspot.com)
STORY:MJUKUU WA MSUKULE PART(20)
Reviewed by Unknown
on
Juni 10, 2017
Rating:
Post a Comment