Header AD

STORY: MJUKUU WA MSUKULE (PART21)


                                         mainfo93.blogsport.com

STORY:MJUKUU WA MSUKULE PART (21)

STORY:MJUKUU WA MSUKULE
PART(21)
MWANDISHI:AMANI ZABRANCO
Facebook page  mainfo93

mainfo93.blogspot.com  Walipofika  jikoni saguda hakuamini macho yake kuona masufuria makubwa yakiwa yamejaa vipande vya nyama za binadamu,saguda akawaona wapishi wakiwa wanapakua nyama za watu kwa kutumia viganja vya binadamu wakiwa wanatumia kama ndo kijiko cha kupakulia. Mmoja wa wapishi akasikika akisema “cheche!!!!! Nyama ya leo ina chumvi mingi sana, inaonekana huyu mtu alikuwa ana afya nzuri’’.
 Saguda akajawa hofu 
kusikia yale maneno ya Yule mpishi, wapishi wakawa wanamshangaa sana saguda kua amewezaje kuingia hadi jikoni. Mpishi mmoja akataka kumpiga saguda na kipande cha mti lakini Yule kikongwe akamkataza akasema yeye ndiye aliyekuja nae mule jikoni.
Yule kikongwe akamuambia saguda amfuate kwa nyuma, hadi wakaingia sehemu ya chumba kingine , saguda akashangaa kuona kuna masufuria mengine yakiwa yanapikwa , alipoyasogelea hakuamini macho yake kuona nyeti za binadamu zikikaangwa kwenye yale masufuria. Yule bibi akamuambia kuwa kile chakula ni cha wakuu wa wachawi ili wapate nguvu za ajabu.
Yule bibi akampeleka saguda hadi kwenye chumba kingine wakakuta mapipa yakiwa yamejaa damu za watu,Saguda akataka kukimbia lakini Yule bibi akamuambia asiwe na wasiwai yeye atamlinda, kikongwe akamuambia saguda kua  zile damu zinatokana na ajari mbalimbali ambazo hua wanazisababisha wao kwa lengo la kupata damu.

Akaendelea kusema kuwa misukule ndio hua wanafanya hiyo kazi, kikongwe akampeleka saguda kwenye chumba cha ndani zaidi ambapo kulikua na mwanga mwekundu ndani yake, saguda akashtuka kuona mitungi mikubwa ikiwa imefunikwa, Yule bibi akafunua mtungi mmoja ili saguda aone kilichomo ndani.

Saguda akajawa na woga mithiri ya mtu aliyenusurika kupata virusi, saguda akachungulia ndani ya mtungi huku akijawa na wasiwasi akaona kuna………….(itaendelea kesho katiaka mainfo93.blogspot.com)

STORY: MJUKUU WA MSUKULE (PART21) STORY: MJUKUU WA MSUKULE (PART21) Reviewed by Unknown on Juni 10, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads