Header AD

Kala kupitia wimbo ‘Wanandoto’ atunukiwa cheti cha heshima na Shirika la Society Watch

kala

Msanii wa muziki wa hip hop, Kala Jeremiah ametunukiwa cheti ya heshima na Shirika la Society Watch kutokana na wimbo wake ‘Wanandoto’ ambao unatetea watoto yatima na
wale wanaoishi katika mazingira magumu
Kala amelishukuru shirika hilo huku akidai hatua hiyo ni nzuri katika muziki wake.
“Kwanza nimshukuru mwenyezi mungu kwa kila alitendalo juu yangu. Pia niwashukuru sana mashabiki wangu kwa kuniamini siku hadi siku. Niwashukuru sana watu wa habari maana bila nyinyi nisingeandika hata huu ujumbe. Lakini kwa namna ya kipekee kabisa niwashukuru sana watu wa Shirika la Society Watch kwa kunipa heshima kubwa sana ya kunitunuku cheti hiki kama njia ya kutambua na kuthamini nilichokifanya kupitia wimbo wangu wa ‘Wanandoto’ unaotetea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu. Hakika cheti hiki ni kitu kikubwa sana kwangu na kwa muziki wangu. Nanicheti changu cha kwanza kabisa. Heshima hii ni kubwa sana. Nasema asanteni sana,” aliandika Kala Jeremiah.
Wanandoto ni wimbo ambao umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na runinga huku kupitia mtandao wa YouTube ukiangaliwa mara 223,547 kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Kala kupitia wimbo ‘Wanandoto’ atunukiwa cheti cha heshima na Shirika la Society Watch Kala kupitia wimbo ‘Wanandoto’ atunukiwa cheti cha heshima na Shirika la Society Watch Reviewed by Unknown on Septemba 22, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads