NIKOHURUBLOG# (AFYA) hiki ndicho kinachopelekea kutokupevuka kwa mfumo wa uzazi
Hili ni tatizo linawakuta walio wengi sana hasa wanawake karibu sasa hii iko hivi. Hali hii hutokana na viungo vya uzalishaji wa vichocheo vya uimarishaji uzazi kwa mwanamke na mwanaume kutofanya kazi. Viungo au Glandi hizi ni korodani kwa mwanaume na ovari kwa mwanamke.
Tatizo hili linaweza kuwa linatokea tangu kuzaliwa au linatokea katika mfumo mzima wa mwili. Kwa tatizo la kuzaliwa nalo, korodani au vifuko vya mayai huwa havifanyi kazi ya kuzalisha vichocheo au homoni zinazohitajika ambapo kwa korodani huzalisha homoni za kiume na ovari huzalisha homoni za kike.
Vyanzo vya matatizo ni kama vile:-
– Matatizo katika mfumo wa kinga mwilini.
– Matatizo katika mfumo wa vinasaba.
– Matatizo ya ini na figo.
DALILI ZA TATIZO
Dalili kwa mtoto wa kike ambaye hajavunja ungo, utamwona bado ni mtoto yaani habadiliki yupo vilevile tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi hadi anafikisha ishirini, matiti hayakui, urefu haongezeki. Kama tatizo likitokea baada ya kuvunja ungo huhisi joto muda wote hata kama kuna baridi, nywele sehemu za siri na makwapani hupuputika zenyewe, hupoteza hamu ya tendo la ndoa kabisa na haendelei tena kupata siku zake na kufunga hata zaidi ya mwaka.
Ukiwa na dalili hizo, muone daktari kwa ushauri zaidi.
NIKOHURUBLOG# (AFYA) hiki ndicho kinachopelekea kutokupevuka kwa mfumo wa uzazi
Reviewed by Unknown
on
Novemba 22, 2016
Rating:
Post a Comment