Picha: Rais Magufuli Alivyoongoza wananchi wa Dar kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 10 Novemba, 2016 aliwaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Waziri na mbunge Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph James Mungai katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Rais Magufuli Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Marehemu Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu, Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu. Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali na Siasa.
Joseph James Mungai alifariki dunia tarehe 08 Novemba, 2016 katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua ghafla na mwili wake utasafirishwa leo Ijumaa kwenda Mafinga Mkoani Iringa kwa Mazishi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa pamoja na waombolezaji wengine walipofika kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016
Picha: Rais Magufuli Alivyoongoza wananchi wa Dar kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai
Reviewed by Unknown
on
Novemba 11, 2016
Rating:
Post a Comment