Header AD

Diamond Platnumz Kuingiza Sokoni Muda Wowote 'Chibu Perfume



Chibu Perfume za mkali wa wimbo Salome, Diamond Platnumz zitaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa kwa mujibu wa Sallam, meneja wa masanii huyo.


Mwaka 2016 muimbaji huyo alionyesha sample ya perfume hizo hali ambayo ilileta shauku kumbwa kwa mshabiki wa muimbaji huyo.

Ijumaa hii meneja wa msanii huyo, kupitia ‘Insta Live’ amedai tayari mzigo wa perfume hizo umeshaingia mjini na utapatikana katika maduka mbalimbali nchini.

“Mzingo umeingia, utapatikana kila sehemu bado hatujapanga bei,” alisema Sallam huku akionyesha perfume hizo.

Meneja huyo alidai perfume hizo hazitapatikana kwa bei ya chini ya laki moja na huwenda bei ikaongezeka kutokana na ubora manukato hayo.

 Jiunge Nasi  >> Facebook <<  >> Instagram <<
Diamond Platnumz Kuingiza Sokoni Muda Wowote 'Chibu Perfume Diamond Platnumz Kuingiza Sokoni Muda Wowote 'Chibu Perfume Reviewed by Unknown on Januari 21, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads