Header AD

“KIJEBA” Wa Congo Aitwa Tena Na CAF. Ni Yule Aliyecheza Dhidi Ya Serengeti Boys.


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF), limewapa  nafasi ya kujitetea ya mwisho kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Congo (FECOFOOT) wakitakiwa kumpeleka mchezaji wao Kijeba, Langa Lesse Bercy jijini Libreville, Gabon kwa ajili ya
kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake. Hii ni baada ya kikao cha kamati kuu kilichofanyika jana Alhamisi.
CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo huko Libreville, Gabon ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12, 2017. Hii ni baada ya hapo kabla kumwita mchezaji huyo mara mbili na FECOFOOT hawakuweza kumpeleka.
Hii ni baada ya malalamiko ya TFF kuwa chama hicho kilikiuka kanuni za mashindano ziliwowekwa na CAF kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya kumchezesha Langa Bercy ambaye walidai kazidi umri. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya kimataifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, vijana waliohitajika kucheza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 17.
Fainali za vijana zinatarajiwa kufanyika katika nchi nyingine itakayotangazwa hapo baadaye baada ya Madagascar kuondolewa kuandaa fainali hizo baada ya kubainika kutokamilisha baadhi ya taratibu.
Hii inatokana na ripoti ambayo CAF wameipata kutoka kwa wakaguzi wa maandalizi ya fainali hizo. CAF imefungua kandarasi ya kwa nchi wanachama wengine kuandaa fainali hizo. Mwisho wa kupokea maombi ni Januari 30, mwaka huu.


“KIJEBA” Wa Congo Aitwa Tena Na CAF. Ni Yule Aliyecheza Dhidi Ya Serengeti Boys. “KIJEBA” Wa Congo Aitwa Tena Na CAF. Ni Yule Aliyecheza Dhidi Ya Serengeti Boys. Reviewed by Unknown on Januari 14, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads