Header AD

Namna Mchezo wa Ku Bet Unavyofanana na Matumizi ya Madawa ya Kulevya

Madawa ya kulevya ni addictive kwa sababu mtumiaji anapotumia kwa mara ya kwanza kuna raha kubwa anaipata anapoyatumia kwa mara ya kwanza

Baada ya kuipata hii raha basi atajaribu kutumia tena madawa haya kuitafuta ile raha aliyokuwa ameipata mwanzo.
.lakini huwa haipati raha kama ya mwanzo, na inampelekea kuongeza kiasi cha dozi kila mara akijaribu kuitafuta na kuirudia rudia hadi anaharibikiwa kabisa

Kwenye ku bet sasa..
kutokana na kuwa na marafiki wa kiume wanao bet nime observe kubet nako ni sawa na matumizi ya narcos tu

Kubet na kwenyewe kunaleta furaha kubwa sana endapo yule anaye bet atafanikiwa kupatia utabiri wake na kushinda fedha nyingi

Ule mshawasha wa kusubiria matokea na kisha utabiri wako kutimia kunaleta excitement kubwa kwa mcheza kamari

Sasa mcheza kamari anaposhinda hupata furaha kubwa na pia kujiamini kuwa yeye ni mtaalamu kwenye kubashiri

Kwa hiyo ataendelea kucheza kamari kwa sababu ya furaha ya kupata pesa za bure kutoja kwenye mchezo anaoupenda na kujiamini ni mtaalamu

Na kwa kuwa mchezo wa kamari upo based kwenye kanuni za probability ambazo zinampa nafasi kwa mchezaji na mwenye kampuni nafasi za kushindaa lakini chances za mcheza kamari kushinda always zinakuwa ni ndogo kuliko za kampuni...yaani hazipo 50%/50%, ni lazima mchezaji ataumia tu in the long run

Na kwa kuwa saikolojia yake ishaathirika yeye anajua atashinda kesho kama akikosa leo kwa kuwa keshashinda mwanzo

atacheza atashindwa ila hata akimaliza fedha yake atakopa ili airudishe fedha yake aliyopoteza

so atashinda na kushindwa (lakini atashindwa mara nyingi zaidi kwa kuwa odds always zinakuwa favourable kwa betting company)

so mwisho wake atauza hata mali zake kupata fedha ya kamari kama hana self control na ku realise kuwa yeye ni ndiye loser kwenye huu mchezo


By Chinchilla Coat/JF
Namna Mchezo wa Ku Bet Unavyofanana na Matumizi ya Madawa ya Kulevya Namna Mchezo wa Ku Bet Unavyofanana na Matumizi ya Madawa ya Kulevya Reviewed by Unknown on Januari 13, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads