Watu 11 waliowahi kutembea kwenye Mwezi
Mpenzi msomaji kumbuka kuwa Mtu wa mwisho kutembea kwenye Mwezi, Gene Cernan, alifariki dunia mapema wiki hii akiwa na umri wa miaka 82.
Basi leo wacha tuangazie list ya binadamu walofika mwezini,
Mtu wa kwanza alikuwa kamanda wa chombo cha safari za anga za juu cha Apollo 17 mwaka 1972 na miongoni mwa watu watatu waliofika mwezini mara mbili
Mtu wa kwanza alikuwa kamanda wa chombo cha safari za anga za juu cha Apollo 17 mwaka 1972 na miongoni mwa watu watatu waliofika mwezini mara mbili
Lakini kuna watu wengine 11 waliomtangulia kufika na kuukanyaga Mwezi. Ni nani hao?
Neil Armstrong (1930 - 2012) na Edwin 'Buzz' Aldrin (alizaliwa 1930)
Armstrong ni maarufu sana kwa maneno yake baada ya kuwa mtu wa kwanza kuukanyaga Mwezi: "Hatua moja ndogo kwa mwanamume mmoja, hatua moja kubwa kwa binadamu."
Wakiwa kwenye Mwezi, Neil na Buzz waliweka bendera ya Marekani na kuacha bango lililokuwa na ujumbe, "Hapa, wanaume kutoka sayari ya Dunia walikanyaga Mwezi kwa mara ya kwanza Julai 1969, AD (Baada ya Kuzaliwa kwa Yesu). Tulifika sote hapa kwa amani kwa niaba ya binadamu wote."
Charles 'Pete' Conrad (1930 - 1999)
Apollo 12 ilipaa angani kukiwa na tufani na radi, hali iliyosababisha nguvu za umeme kuzimika muda mfupi baada yao kuruka angani.
Conrad mwishowe alipoukanyaga Mwezi, alisema kwa sauti: "Whoopee! Bwana, hiyo huenda ilikuwa hatua ndogo kwa Neil, lakini kwangu imekuwa kubwa sana."
Alan L Bean (alizaliwa 1932)
Bean ni msanii pekee ambaye amewahi kusafiri nje ya sayari ya dunia.
Michoro na picha zake kwa hivyo zina uhalisia fulani kuhusu hali ilivyo kwenye Mwezi.
Alan Shepard (1923 - 1998)
Shepard anakumbukwa kwa kupiga mipira kadha ya gofu kwenye Mwezi akitumia kipande kidogo cha chuma.
Kutokana na kiwango cha chini cha nguvu mvutano (graviti), mipira hiyo ilikwenda mbali sana kuliko inavyowezekana kwenye Dunia.
Edgar D Mitchell (1930 - 2016)
Mitchell alikuwa binadamu wa kwanza kupeperusha picha za runinga za rangi kutoka kwenye Mwezi. Alibeba pia jiwe la uzani wa kilo 43.5 kutoka mwezini pamoja na mchanga na akarejea navyo duniani.
David Scott (alizaliwa 1932)
Scott ni maarufu sana kutokana na stempu zake.
Bila idhini ya Nasa, alisafiri na stempu za posta hadi mwezini akiwa na mpango wa kuziuza baada ya kurejea nazo duniani. Hakusafiri anga za juu tena.
James B Irwin (1930 - 1991)
Irwin alipokuwa safarini, maafisa ardhini waligundua alikuwa akikabiliwa na matatizo ya moyo.
Lakini kwa sababu alikuwa akipumua oksijeni asilimia 100 na nguvu mvuto huko kwenye Mwezi zilikuwa chini, waliamua hakuwa hatarini.
Mpigo wa moyo wake ulirejea kawaida aliporudi duniani.
Hata hivyo, alifariki kutokana na mshtuko wa moyo miezi kadha baadaye.
John Young (alizaliwa 1930)
John Young ndiye mwana anga aliyehudumu muda mrefu zaidi katika historia ya Nasa, kufikia sasa.
Wakati mmoja, aliingia na kipande cha mkate kilichotiwa mboga kwenye chombo cha anga za juu safarini.Wakuu wa Nasa hawakufurahishwa na hilo. Lakini Young aliendelea na kazi na alisafiri anga za juu mara sita.
Charles M Duke Jr (alizaliwa 1935)
Duke aliweka historia alipougua surua wakati wa mafunzo ya wahudumu wa ziada wa Apollo 13.
Aliwaweka hatarini wahudumu na kulazimisha mmoja wa wana anga kubadilishwa.
Harrison 'Jack' Schmitt (alizaliwa 1935)
Schmitt alikuwa mwanasayansi wa kwanza kwenda anga za juu.
Alikuwa kwenye Apollo 17 na alikaa siku tatu kwenye Mwezi akiwa na Gene Cernan.
Alirusha nyundo pekee waliyobeba mbali na pia aliacha vifaa vyake vya kupimia kwenye Mwezi.
Watu 11 waliowahi kutembea kwenye Mwezi
Reviewed by Unknown
on
Januari 21, 2017
Rating:
Post a Comment