Header AD

Wolper Awatolea Povu Mastaa Wenzake,Adai ni Washamba,Kisa Ni...!!!


STAA wa filamu za Bongo, Jackline Wolper, amesema sasa hivi ameamua kuanza maisha ya kistaa kwa kutoanika mambo yake binafsi kwenye mitandao ya kijamii, kwani aliyokuwa anafanya mwanzo ilikuwa ni ushamba.


Akizungumza , Wolper alisema kwa muda mrefu ameishi maisha ya kishamba kwa kuanika mambo yake binafsi kwenye mitandao badala ya kuitumia kutangaza kazi zake za filamu.

“Kiukweli sasa nimeelimika na nimejijua kama mimi ni staa na ninapaswa kuishi kistaa, sitarusha chochote kile kinachohusu maisha yangu kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Wolper.

Msanii huyo alisema mastaa wa Kibongo wamekuwa washamba na mitandao hiyo kwani wameshindwa kuitumia kibiashara kama wanavyofanya wenzao kutoka nchi nyingine duniani.
Wolper Awatolea Povu Mastaa Wenzake,Adai ni Washamba,Kisa Ni...!!! Wolper Awatolea Povu Mastaa Wenzake,Adai ni Washamba,Kisa Ni...!!! Reviewed by Unknown on Januari 15, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads