Aliyekuwa mfungwa ndio waziri wa fedha Gambia
Rais Adama Barrow wa Gambia
Miongoni mwa wafungwa walioachiliwa huru hivi karibuni nchini Gambia, ni miongoni mwa watakaounda baraza jipya la mawaziri , chini ya utawala wa raisi wa sasa Adama Barrow.
Amadou Sanneh, alifungwa kwa tuhuma za kuonekana ni mpinzani wa kisiasa wa kiongozi wa zamani Yahya Jammeh, katika baraza jipya ameteuliwa kushika wadhifa wa waziri wa fedha saa sabini na mbili mara baada tu ya kuachiliwa huru.
Mawaziri wengine tisa wamekwisha kula kiapo chao, akiwemo waziri mpya wa mambo ya nje wa Gambia , Ousainou Darboe,ambaye naye alikuwa mpinzani mkubwa wa utawala wa bwana Jammeh , ambaye pia alishawahi kufungwa na utawala uliopita.
Mawaziri wengine nane ambao bado hawajajaza nafasi katika baraza la mawaziri bado hawajafahamika.
Jammeh alikuwa mamlakani tangu mwaka 1994, aliondoka nchini Gambia na kuelekea uhamishoni mwezi uliopita kufuatia kushindwa kwa uchaguzi uliofanyika mwezi December mwaka wa jana na Adama Barrow kuibuka mshindi.
CREDIT: BBC
Aliyekuwa mfungwa ndio waziri wa fedha Gambia
Reviewed by Unknown
on
Februari 02, 2017
Rating:
Post a Comment