Header AD

Wakongo washtushwa na kifo cha Tshisekedi

Etienne Tshisekedi, akihutubia mkutano wa upinzani Kinshasa Julai 9 2005.
Kiongozi wa upinzani wa muda mrefu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi afariki akiwa na umri wa miaka 84 alipokua mjini Brussels kuonana na madaktari wake.

Msemaji wa chama chake cha UDPS alithibitisha Jumatanoi kwa Sauti ya Amerika kwamba kiongozi hiyo alipimwa na daktari wake, na kueleza kwamba hana matatizo makubwa ya Afya, lakini kifo chake kilitokea ghafla muda mfupi baadae.
Wafuasi wake mara moja walikusanyika nyumbani kwake na kwenye makao makuu ya chama cha UDPS, kwa mshangao na usikitifu. Kuna baadhi wanasema walikuwepo aliposafiri Januari 24 kuelekea Brussels kwa matibabu, na waliona alikua na afya yake ingawa ni mtu mzima.
Tshisekedi alianza siasa akiwa na wapiganaji wa uhuru wa Kongo kabla ya kua waziri katika serikali ya rais wa zamani Mobutu Seseseko, kabla ya kuunda chama cha UDPS, chama cha kwanza cha upinzani huko Zaire mwaka 1982.
Baada ya hapo alichaguliwa mara nne kua waziri mkuu chini ya Mobutu miaka ya 1990, wakati kiongozi huyo alipojaribu kuanzisha mfumo wa kidemokrasia nchini. Lakini mara hizo zote hakuweza kubaki muda mrefu katika cheo hicho kutokana na kugombana na kiongozi huyo wa utawala wa kimabavu.
Baada ya Mobutu kuondolewa madarakani 2001, kutokana na msaada wa Rwanda na Uganda na vikosi vingine vilivyomleta madarakani Laurent Kabila, Tshisekedi akajikuta tena kua mpinzani mkubwa wake na baadae mpinzani mkuu wa mtoto wake Joseph.
Akizungumza na sauti ya amerika mwaka 2011 wakati wa ghasia yaliyotokea kupinga uchaguzi wa Josepoh Kabila, alipotokea wa pili, Tshisekedi alisema hajaamrisha watu kujtumia nguvu kugombania haki zao.
Etienne Tshisekedi, akihutubia mkutano wa upinzani Kinshasa Julai 9 2005.
Etienne Tshisekedi, akihutubia mkutano wa upinzani Kinshasa Julai 9 2005.
Sijajuta hata kiogo ni haki ya wakongo kutetea haki yao na kupigania haki zao kwa njia ya Amani. Mimi sijamrisha wafuasi wangu kutumia silaha bali nimewambia wakusanyike kwa pamoja kupinga matokeo ya ucahguzi wa dikteta.
Amri ya maandamano makubwa ya upinzani daima yamekua yakiongozwa na Tshisekedi, na anasifiwa kwa kuweza kuunganisha upinzani kupinga jaribio la Rais Kabila kubaki madarakani baada ya muda wake kumalizika mwezi disemba mwaka jana.
Msemaji wa vuguvugu la serikali Henri Mova akizungumza na Sauti ya Amerika anasema taifa limempoteza shujaa.
Taifa limempoteza mwanasiasa mkgonwe mashuhuri. Na si upinzani pekee ulompoteza kiongozi wao, bali nchi nzima kwani Tshisekedi ni mtu aliyeanza vita vya kisiasa tangu wakati wa kupigania uhuru na inabidi kutambua kwamba alileta mabadiliko makubwa katika siasa za Kongo. Kwa hivyo tunaweza kusema huu ni mwisho wa enzi muhimu ya siasa za nchi hii.
Mtoto wa Tshisekedi Felix anatajwa huwenda akawa waziri mkuu wa utawala wa mpito. Wakiongo wameanza kueleza usikitifu wao na matayarisho yananaza kupokea mwili wake kutoka Brusselss. Wakuu wa UDPS wanasema uchunguzi unafanyika kuweza kujua nini hasa kiilicvhosababisha kifo chake.
Wakongo washtushwa na kifo cha Tshisekedi Wakongo washtushwa na kifo cha Tshisekedi Reviewed by Unknown on Februari 02, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads