Header AD

Walio faulu kidato cha kwanza kurudia mtihani tareh 28 February

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema 
wanafunzi ambao walichaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza katika shule za serikali nchini wanahitajika
kufanya mtihani wa udahili tarehe 28 mwezi huu
na
wale watakaofaulu wataruhusiwa kujiunga na kidato
hicho.

Taarifa hii ilitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu
Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt.
Charles Msonde lakini kwa mujibu wa barua kutoka
NECTA iliyosainiwa na Edgar Kasuga kwa niaba ya
Katibu Mkuu kwenda kwa Makatibu Tawala wote wa
Tanzania Bara siku ya Jumatatu, wale ambao
hawatafaulu hawataruhusiwa kuendelea na masomo
hayo ya sekondari.

NECTA inakusudia kutumia mtihani huo kuhakiki
uwezo wa wanafunzi waliounesha katika kiwango chao
cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu
ya Msingi uliofanyika mwaka jana. “Watakaofeli
hawataruhusiwa kuendelea na masomo,” inasomeka
sehemu ya barua hiyo. Makatibu Tawala wote, maafisa
elimu na walimu wakuu wote wa shule za sekondari za
serikali waliombwa kufikia leo wawe wamewasilisha
orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na shule zao ili maandalizi yafanyike.

Afisa mmoja wa NECTA amesema maandalizi kwa ajili
ya mtihani huo yanaendelea na kwamba wanafunzi
wajiandae. “Maandalizi yanaendelea vizuri na tutatoa
taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko yoyote
yatakayojitokeza,” alisema.

SOURCE: ITV

Walio faulu kidato cha kwanza kurudia mtihani tareh 28 February Walio faulu kidato cha kwanza kurudia mtihani tareh 28 February Reviewed by Unknown on Februari 12, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads