NIKOHURU BLOG#Tazama hapa miaka 20 ya mitindo ya nywele na mbunifu Marc Jacobs
Mbunifu wa mavazi kutoka marekani Marc Jacobs aonesha historia ya mitindo ya nywele kupitia wana mitindo wake ambao aliwavalisha kulingana na
miaka yote aliofanya ubunifu wake kuanzia mwaka 1996 mpka leo, huku akichukua kofia ya mbunifu bora wa mwaka katika mitindo ya nywele.
Marc Jacobs amesema kwamba amekua akivutiwa na nywele za wanawake hivyo kumpelekea kujihusisha na kutengeneza mitindo mbalimbali ya nywele na kumuwezesha kufanikiwa au kufikia hapa alipo sasa.
“kati ya vitu vinavyompendezesha mwanamke ni nywele hivyo zimekuazikinivutia na kuibuka na mbinumbalimbali kila siku katika kuboresha na kufanya kitu cha tofauti kuvutia watu wengi zaidi.” Amesema Marc
Aidha taarifa zimesema kwamba Jacob amekua akiongoza katika ubunifu bora kwa muda mrefu sasa kupitia kampuni yake ya mavazi iitwayo “marc Jacobs” yenye maduka ya nguo 200 katika zaidi ya nchi 80 duniani, huku akifanya kazi na lebo ya kampuni kubwa ya nguo “lousi Vuitton”.
NIKOHURU BLOG#Tazama hapa miaka 20 ya mitindo ya nywele na mbunifu Marc Jacobs
Reviewed by Unknown
on
Septemba 18, 2016
Rating:
Post a Comment