NIKOHURU BLOG#Hii sio ya kukosa: Angalia hapa best Android Applications za mwaka 2016 mpaka sasa
Kutafuta application nzuri zaidi katika Play Store ni kazi kidogo. Haijalishi iwe app ya afya, hali ya hewa au muziki kwa sababu zipo applications nyingi sana zinazofanya kile unachokihitaji kwa sasa. Leo tumejaribu kuangalia zile applications bora zaidi katika kila nyanja na kujaribu kuzichambua moja moja.
Best File Manager Application
Bado ES File Explorer inaongoza katika orodha ya applications kali zaidi za kubrowse mafaili. Ikiwa na uwezo wa kuunganisha simu yako na laptop yako kupitia wifi, kucheza miziki na video za kwenye pc yako kupitia kwenye simu yako bila ya kuzisave, uwezo wa kumanage kila kitu katika vifaa vyako bila tabu yoyote ule kunaifanya ES Explorer kuwa App namba moja katika orodha hii.
Ukiachana na ES File Explorer kuna Solid File Explorer ambayo kwa sasa inafanya vizuri na inakaribiana kila kitu na ES. Kwa kutumia Solid File Explorer utaweza kuweka vitu katika Dropbox, Drive au OneDrive moja kwa moja. Pia unaweza ukazip, RAR au kuhide mafolder katika simu au tablet yako.
Best Launcher Application
Unapozungumzia muonekano mzuri wa kioo cha simu yako kunaendana moja kwa moja na Launcher unayotumia. Mara nyingi watumiaji wengi wa Android hupendelea kuweka Launcher wanazozifurahia kila wanaposhika simu zao.
Hapa ndipo Action Launcher 3 inapoingia. Ikiwa na interfae nyepesi na rahisi kutumia action launcher imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya launcher za android.
Best Application ya Fitness na Mazoezi
Kama wewe ni mpenzi wa mazoezi mazito au mazoezi mepesi mepesi 7 Minute Workout ndio app inayokufaa zaidi. App hii inatilia mkazo katika mazoezi mepesi mepesi yanayojirudia ambayo yamethibishwa kitaalamu kuwa yanasaidia sana katika kupunguza uzito na kukuweka fit masaa yote. Ingia PlayStore uipakue ujionee mwenyewe.
Best Android browser app
Hapa ndipo wengi wanapapenda, kukiwa na msururu mrefu wa browsers au vivinjari kama Operamini, UC Browser, Safari, internet Explorer bado Chrome Beta ndio application bora zaidi katika vivinjari. Wepesi wa kuvinjari kunakifanya kivinjari hiki kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani kwa sasa kuliko kivinjari kingine chochote kile.
Best Music Play app
Moja ya mahitaji makubwa ya simu ni kusikiliza muziki, mziki mzito siku zote unategemea vitu vikuu vitatu;aina ya simu unayotumia, aina ya spika au earphones pamoja na app unayotumia kupigia huo mziki. Baada ya kutest apps tofauti tofauti za kuplay music swahilitech tukapata app tano bora katika kusikiliza music.
Hebu tuiangalie orodha yenyewe inavyofanana,
1. Power Amp; Power Amp imeendelea kuwa app bora kabisa ya kusikilizia music katika simu za android. Ikiwa na huduma nyingi kama equalizer, basebooster na amplifier inayoeleweka power amp imeshika nafasi ya kwanza katika orodha hii. Unaweza ukaipakua kutoka playstore.
2. Google Play Music; Hapa nadhani bila shaka utakubaliana na mimi hii app ni bora kabisa kwa sasa. Ikiwa na uwezo wa kukuwezesha kusikiliza redio za mtandaoni kiurahisi, kustream mziki kutoka sehemu mbalimbali pamoja na kukuwezesha kusikiliza music katika simu yenye uwezo wowote ule tofauti na apps nyingine.
3. Jet Audio; Jet Audio imeondolewa katika nafasi ya pili na Google Play Music lakini bado inabaki kuwa app bora kabisa kwa wale wanaopenda kusoma lyrics huku wanasikiliza music. Ikiwa na uwezo kama wa PowerAmp Jet Audio bado inafanya vizuri sokoni. Unaweza ukapakua toleo la bure kutoka google Play.
4. Black Player; App hii sio maarufu ila imeingia kwa kasi katika orodha yetu kwa kuwa ndio app pekee ya bure ukiacha Google Play Music inayotoa huduma nyingi za bure kwa mtumiaji wake. Hutojutia kutumia app hii kama wewe unapenda mziki mnene.
5. N7 Music Player; Hawa jamaa wanafanya vizuri katika fani hii ya apps za music. Ikiwa na uwezo mkubwa wa kuchuja na kuamplify music N7 Music Player inaingia kwenye orodha ya App bora zaidi za muziki.
Usikose uchambuzi wa Apps za Android na iOS toleo la pili, usisahau ku"share habari zetu kwa rafiki zako
Toa maoni yako
NIKOHURU BLOG#Hii sio ya kukosa: Angalia hapa best Android Applications za mwaka 2016 mpaka sasa
Reviewed by Unknown
on
Septemba 18, 2016
Rating:
Post a Comment