NIKOHURU BLOG#Samsung wanapaswa kupongezwa kwa hatua ilizochukua baada ya Note 7 kulipuka
Ni wiki ya pili sasa tangu Samsung kusitisha mauzo ya Samsung Galaxy Note 7 kwa sababu ya kuripotiwa kwa matukio 35 ya kulipuka kwa betri za simu hizo. Je, Samsung ni kampuni ya kwanza kuchukua hatua kama hizo katika soko?
Hii imetokea mapema sana baada ya simu hii ambayo ilionekana kuteka mioyo ya mashabiki wengi wa simu kutoka kampuni ya Samsung kuripotiwa kuwa ina matatizo katika betri na kusababisha milipuko.
Hii imetokea mapema sana baada ya simu hii ambayo ilionekana kuteka mioyo ya mashabiki wengi wa simu kutoka kampuni ya Samsung kuripotiwa kuwa ina matatizo katika betri na kusababisha milipuko.
Je, hii ni mara ya kwanza katika soko?
Mwaka 2010 kampuni ya Apple ilitambulisha rasmi simu zake za iPhone 4 mwezi June. Baada ya kuingia tu sokoni watumiaji wengi wa simu hizi walianza kulalamikia uwezo wa simu hizi kushika mawimbi ya mtandao. Simu nyingi zilikuwa zikipoteza mtandao katikati ya maongezi.
Kipindi hicho, Apple ilikuwa ikiongoza soko la smartphones na iligoma kukubali suala hilo na kudai watumiaji wa simu hizo walishindwa kuzishika vizuri.
Ilipofika July 2, Apple walitoa kauli rasmi kuhusiana na tatizo hilo na kudai formula waliyotumia kukokotoa kiasi cha mawimbi ya mtandao kinachopokelewa na wingi wa bars zinazoonekana kuwakilisha network ilikosewa na kuleta matatizo hayo.
Baadhi ya watumiaji walikubaliana na hilo ila baadhi waliendelea kulalamikia bidhaa hiyo kutoka Apple. Baada ya wiki mbili CEO wa Apple wa kipindi hicho bwana Steve Jobs alithibitisha kuwepo tatizo hilo na kudai ni tatizo dogo la kiufundi. Apple wakatangaza kutoa makava ya simu hizo yanayoweza kuboost mawimbi ya mtandao bure kwa watumiaji wote wa iphone 4 na kuwafidia wale ambao walishanunu makava hayo kwa pesa zao.
Hali ilivyo kwa Samsung
Baada ya kuripotiwa kwa visa 35 vya kulipuka kwa betri za Samsung Galaxy Note 7 ambayo ilikuwa na wiki mbili tu sokoni kampuni ya Samsung ilitangaza kusitisha mauzo yote ya simu hizi na kuwataka wateja wote ambao walishazinunua kuzirudisha ili kupewa toleo lililosalama.
Huu ni ukomavu wa hali ya juu ulionyeshwa na kampuni kutoka Korea Kusini licha ya kuathiri kwa kiasi kikubwa soko lako kwa sasa. Katika nusu ya mwaka 2016 Samsung ilionekana kufanya vizuri katika soko hasa kwa kuachia Samsung Galaxy S7 na S7 Edge ambazo ziliibuka kuwa mpinzani mkali wa Apple iPhone 6.
Kama mdau wa teknolojia na gadjets toa maoni yako juu ya hatua hii iliyochukuliwa na Samsung.
#MAKALA:Kwa hisani ya swahiliTech.
#MAKALA:Kwa hisani ya swahiliTech.
Toa maoni yako
NIKOHURU BLOG#Samsung wanapaswa kupongezwa kwa hatua ilizochukua baada ya Note 7 kulipuka
Reviewed by Unknown
on
Septemba 18, 2016
Rating:
Post a Comment