Header AD

NIKOHURU BLOG#Utafiti: Kulala zaidi ya saa 1 mchana kunaongeza hatari ya kuugua kisukari

woman-asleep-at-computer
Kupata walau saa moja ya kuuchapa usingizi mchana, ni tamanio la wafanyakazi wengi walio busy.
Lakini timu ya wanasayansi imeonya kuwa kujiruhusu kupata lepe refu la usingizi mchana kunaweza kukuongezea hatari ya
kupata ugonjwa wa Kisukari. Wamesema wale wanaolala kwa zaidi ya saa moja kwa siku, wana asilimia 45 ya kupata ugonjwa huo mbaya, watafiti wamebaini.
Hata hivyo kulala kwa muda mfupi, hakukuonesha hatari zozote, kwa mujibu wa utafiti huo uliowasilishwa kwenye mkutano wa Umoja wa Ulaya kwa tafiti za kisukari, (EASD) huko Munich, Ujerumani.
Wataalam kutoka Japan, waliangalia taarifa kutoka tafiti 21 zilizohusisha watu 300,000 na kukuta uhusiano kati ya ulalaji wa mchana na kisukari. Waligundua kuwa kulala kwa zaidi ya saa nzima kunawaweka watu katika hatari ya kuupata ugonjwa huo.
Lakini wale wanaolala chini ya saa moja, hawakuwa kwenye hatari hiyo.
Walielekeza pia kuwa kulala vizuri ni sehemu muhimu ya maisha yenye afya pamoja na chakula bora na mazoez
NIKOHURU BLOG#Utafiti: Kulala zaidi ya saa 1 mchana kunaongeza hatari ya kuugua kisukari NIKOHURU BLOG#Utafiti: Kulala zaidi ya saa 1 mchana kunaongeza hatari ya kuugua kisukari Reviewed by Unknown on Septemba 16, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads