NIKOHURU BLOG#VITAMBULISHO VYA TAIFA KUTUMIKA KATIKA UCHAGUZI UJAO
VITAMBULISHO vya Taifa huenda vikatumika katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Rose Mdami wakati akitoa maelezo kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa bungeni mjini hapa katika hafla ya kumkabidhi kiongozi huyo wa Bunge kitambulisho chake cha taifa.Mdami alisema tayari mamlaka hiyo imechukua taarifa za wapigakura kutoka kwenye kanzidata ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuzichakata na kuna uwezekano mkubwa vitambulisho vya taifa vikatumika katika uchaguzi ujao na kuirahisishia kazi tume hiyo kufanikisha uchaguzi huo wa Rais, Wabunge na Madiwani.
“Vitambulisho tunavyovitoa sasa vina saini ya mtu husika, hivyo vitatumika benki. Tumewashirikisha pia NEC ambao wametupa ‘database’ (kanzidata) yao, tumezichakata na tunaendelea na taratibu ili ikiwezekana Vitambulisho vya Taifa vitumike katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 badala ya vile vya tume,” alisema Mdami.
NIKOHURU BLOG#VITAMBULISHO VYA TAIFA KUTUMIKA KATIKA UCHAGUZI UJAO
Reviewed by Unknown
on
Septemba 16, 2016
Rating:
Post a Comment