NIKOHURU BLOG#Wataalam wa maabara waagizwa kujisajili
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza waajili wote nchini kutoajili wataalamu wasio sajiliwa na wataalamu wa Baraza la Maabara za Afya nchini ili kuepuka kuajili wataalam hewa.
Dk. Kigwangalla ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wataalamu wa Huduma za Maabara za Afya tukio lililofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Naibu Waziri alikuwa mgeni rasmi huku akitoa vyeti kwa wajumbe wa Baraza hilo waliomaliza muda wao pamoja na wajumbe wapya.
Akipongeza Baraza hilo la Maabara, alisema kuwa licha ya kuwa ni la siku nyingi, amelitaka kuhakikisha wanashirikiana na Mamlaka zingine husika kusimamia ubora wa wataalamu kusimamia vyuo husika katika kuwapata wataalam hao.
Pia aliwataka wataalamu wa Maabara waliosajiliwa kwa sheria ya 12 ya 1997, wajisajili tena upya kwa sheria mpya ya namba 22 ya mwaka 2007 kama ilivyoelekezwa ili wapate vyeti vipya.
Mwisho aliwaagiza wataalamu woye wa maabara waliosajiliwa wahakikishe wanalipia ada ya usajili kila mwaka ili kuendelea kupata kibali cha kuendelea kutoa huduma cha maabara kwa mwaka mzima ili baraza hilo liweze kujiendesha.
“Ili muwe wataalam, lazima muwe na chombo kama hichi. Hivyo katika msingi huo nyie wataalum wenyewe mutakiwa kujiongeza katika kuhakikisha munapata fedha kwa kuchangia/kuchangishana muweze kujindesha kama yalivyo mabaraza mengine” alisema Dk.Kigwangalla.
Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya, ni chombo cha kisheria kilichowekwa na Serikali ili kuwatambua na kuwasajili Wataalamu wa Maabara za Afya ya Binadamu, kusimamia ubora wa utoaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya binadamu, kuchukua hatua za kisheria kwa wakiukaji wa sheria, na kushauri Serikali katika kuboresha huduma za maabara kwa wagonjwa.
NIKOHURU BLOG#Wataalam wa maabara waagizwa kujisajili
Reviewed by Unknown
on
Septemba 20, 2016
Rating:
Post a Comment