Rais Magufuli ateua Wenyeviti wa Bodi na Meneja Mkuu Masoko Kariakoo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali kama ifuatavyo;
Kwanza, Rais Magufuli amemteua Prof. Jacob Philip Mtabaji kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuanzia tarehe 15 Septemba, 2016.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali kama ifuatavyo;
Prof. Jacob Philip Mtabaji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Awadhi Mawenya ambaye uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Kamisheni ya TCU kuvunjwa.
Pili, Rais Magufuli amemteua Prof. Mathew L. Luhanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe (MU) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.
Prof. Mathew L. Luhanga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Daniel Mkude ambaye amemaliza muda wake.
Tatu, Rais Magufuli amemteua Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.
Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake.
Nne, Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudensia M. Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.
Bi. Gaudensia M. Kabaka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Augustine Mahiga ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Tano, Rais Magufuli amemteua Bi. Mariam Mwafisi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia 05 Septemba, 2016.
Bi. Mariam Mwafisi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Deogratias Ntukamazina ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Hetson Msalale Kipsi kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Rais Magufuli ateua Wenyeviti wa Bodi na Meneja Mkuu Masoko Kariakoo
Reviewed by Unknown
on
Septemba 20, 2016
Rating:
Post a Comment