Kauli ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa wanaotumia picha zake mitandaoni na kupotosha aliyoyasema
Rais mstaafu kutoka kwenye awamu ya nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kujibu kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii katika siku za karibuni.
Usiku wa kuamkia leo, kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Mstaafu wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete aliandika masikitiko yake juu ya namna watu wanavyotumia picha zake na kupotosha yale aliyoyasema juzi akiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kufanikisha matwaka yao ya kisiasa.
Aidha, Rais Kikwete aliwataka watu hao kumuacha kwani ameshamaliza muda wake wa uongozi hivyo ni wakati wake sasa kupumzika.
Rais Kikwete pia alikanusha tuhuma za kuwa anatofauti na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli pamoja na serikali yake.
Kauli ya Rais Mstaafu Kikwete ambayo imekuwa ikipotoshwa mtandaoni ni ile aliyoitoa kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo aliwataka viongozi wapya kuenzi mazuri ya nyuma akimaanisha kwamba hivi sasa yeye ndo Mkuu wa Chuo hicho(Chancellor), hivyo akaahidi kuyaenzi mazuri aliyoyakuta toka kwa watangulizi wake
“Ukiwa mpya lazima watu waone una mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo," alisema Rais Mstaafu Kikwete na kuongeza; “Sio mapya ya kubomoa ya kule tulikotoka,”
Kauli ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa wanaotumia picha zake mitandaoni na kupotosha aliyoyasema
Reviewed by Unknown
on
Oktoba 28, 2016
Rating:
Post a Comment