Header AD

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya wafungwa baada ya Mtu Mmoja Kuuawa kwa Risasi Nje ya Ubalozi Huo

Jeshi la Polisi jijini Nairobi nchini Kenya linafanya uchunguzi kuweza kubaini kama mtu mmoja aliyeuawa jana karibu na ubalozi wa Marekani alikuwa amekula njama za kushirikiana na watu wengine kufanya shambulio.

Mtu huyo (24) aliuawa jana asubuhi nje ya ubalozi wa Marekani Nairobi baada ya kumshambulia mlinzi kwa kumchoma na kisu tumboni ndipo Afisa mwingine wa Polisi akampiga risasi kichwani.

Inadaiwa kuwa kijana huyo alikuwa akilazimisha kuingia ndani ya ubalozi huo, na mlinzi alipomzuia ndipo akamchoma kwa kisu.

Maafisa watano wa FBI na maafisa wa Polisi nchini Kenya walikuwa karibu na eneo la tukio ambapo ni nje kidogo ya ubalozi wa Marekani.

Tukio hilo limepelekea ubalozi wa Marekani kufungwa kwa muda hadi hapo hali ya usalama itakaporejea katika hali yake.

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya wafungwa baada ya Mtu Mmoja Kuuawa kwa Risasi Nje ya Ubalozi Huo Ubalozi wa Marekani nchini Kenya wafungwa baada ya Mtu Mmoja Kuuawa kwa Risasi Nje ya Ubalozi Huo Reviewed by Unknown on Oktoba 28, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads