Trump ni hatari kwa dunia, anasema afisa wa Umoja wa Mataifa
Maoni ya Donald Trump "yanayokera na kuzusha wasiwasi mkubwa" yanamfanya kuwa tishio kimataifa, Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa mataifa amesema. Zeid Raad al-Hussein ametaja matamshi ya Trump kuhusu kutumia mateso, na msimamo wake dhidi ya 'jamii zilizomo hatarini'.
Kampeni ya mgombea huyo wa chama cha Republican imekumbwa na shutuma kali dhidi ya matamshi yake yanayozusha mzozo.
Mazungumzo yake ya hivi karibuni kuhusu wanawake yamesababisha mgawanyiko mkubwa kisiasa.
Bwana Hussein amesema katika mkutano na waandishi habari Geneva: "iwapo Donald Trump atachaguliwa kwa misingi ya alichokisema tayari - na labda hilo libadilike - nadhani, pasi na shaka anakuwa ni mtu hatari katika matazamo wa kimataifa."
Hussein amesema wakati uchaguzi utasabaisha kushuhudiwa ongezeko la visa vya watu kuteswa "au kulengwa kwa jamii zilizopo hatarini katika namna ambayo itasababisha wanyimwe haki zao za binaadamu, basi nadhani ni muhimu kusema hivyo".
Kamishna huyo amesema hataki kuingilia uchaguzi huo, lakini ana haki ya kuzungumza.
Matamshi ya Trump dhidi ya wahamiaji, hususan raia wanaotoka Mexico, yamezusha hasira kutoka kwa wanaharakati wa kutetea haki za binadamu.
Ameahidi kujenga ukuta katika mpaka na Mexico na mwezi Juni 2015 aliwaita wahamiaji kutoka Mexico "wabakaji" na "wauaji".
Huenda matamshi ya Hussein yasibadili shutuma kali za tajiri huyo wa New York kuhsu Umoja wa mataifa.
"Umoja wa mataifa sio rafiki wa demokrasia," Trump alisema mnamo Machi. "sio rafiki pia kwa hata Marekani, ambako sote tunajua ndio makaazi yake makuu."
Ameishutumu hatua ya Marekani kutenga fedha katika kuendeleza Umoaj huo.
Mwezi Aprili, alisema: "Ni wapi unapo uona Umoja wamataifa? Je unatatua chochote? Ni kama mchezo wa kisiasa. Umoja wa mataifa- namaanisha fedha tunazotumia katika kuendeleza Umoja wa mataifa."
Trump ni hatari kwa dunia, anasema afisa wa Umoja wa Mataifa
Reviewed by Unknown
on
Oktoba 12, 2016
Rating:
Post a Comment