HADITHI: NAYAPENDA MAISHA LAKINI MAISHA HAYANIPENDI
SEHEMU YA (2)
MWANDISHI: ZABRANCO
, lakini kila
herera alipokua anataka kusimama alikua anajikuta akishindwa kwa sababu alikua
kaumia mbavu kutokana na lile teke alilopigwa na yule mkuu wa kile kikundi cha
waasi. Herera akajiburuza hadi pale walipokua wamefia wazazi wake kisha
akaisogelea maiti ya baba yake chozi la huzuni likawa linatanda kwenye uso wa
herera, akaifumba macho maiti ya baba yake kisha akasimama akaisogelea maiti ya mama yake iliyokua
imetapakaa damu kutokana na risasimfururizo alizopigwa maeneo ya kifuani.
Herera akaikumbatia maiti ya mama
yake huku akiwa Analia kwa machungu, akaifumba macho ile maiti huku akiwa
anawaza ni jinsi gani atawazika wazazi wake kwa hua alikua kaumia vibaya mbavu
zake hakua na uwezo wa kusimama wala kutembea akaona njia pekee ya kusaidiwa ni
kupiga kelele kuwaita majirani, lakini akwaza kua watu wa ‘watengwa area’ hua hawatoki nje kipindi wanaposikia
milio ya risasi kwenye kitongoji chao, herea akajaribu kuita watu waje
kumsaidia akaita mara tatu kwa sauti ya juu lakini hakuna hata mmoja
aliyejitokeza kuja kumsaidia hakukata tamaa akaendelea kuita kwa sauti ya juu
huku akisema kua wasiogope tayari waasi wameshaondoka, aliposema hivo ndipo
watu wakaanza kuchungulia kwenye madirisha ya nyumba zao, kweli wakamuona
herera akiwa amekaa pale nje huku kwa pembeni yake kuna maiti mbili. Akatoka
mwanaume mmoja akamsogelea herera pale alipokua amekaa, kisha watu wakazidi
kuchomoza wakitokea ndani ya nyumba zao kama kuku waliofunguliwa kutoka nje y a
banda lao, wakamzunguka herera huku wakisikitika kwa njisi zile maiti za
majirani zao zilivyokua zimeraruliwa kinyama. Wakachukua kanaga wakazifunika
zile maiti kisha wakazichukua na kuzipeleka kwenye nyumba ya kina herera iliyokua
imeezekwa kwa kutumia makuti kwa kua nyuimba yao ya awali ilipigwa bomu miaka
miwili iliyopita pale ambapo kulikua na mapigano makali kati ya waasi na
wanajeshi wa serikali ya nchi ya ‘RED ZONE’.
Nyumba ya kina herera ilikua ikidhihirisha kua
watu wa kitongoji cha ‘watengwa area’ ni masikini wakutupwa kutokana na madhara
ya vita amabayo imekua ikitokea kwa miaka mingi sana. Watu wakakubaliana kua
inabidi wazizike maiti za wazazi wa herera, siku iliyofuata mazishi yakafanyika
kwenye shamba la kina herera lilokua limezagaa mahindi yaliyoharibiwa vibaya
kutokana na waasi kupitisha magari yao ya kivita ndani ya mashamba ya watu wa
kitongoji cha watengwa area. Wazazi wa herera wakazikwa kwenye lile shamba
kisha watu wakatawanyika huku herera akabaki kua yatima akiwa hana shangazi
wala mjomba wala ndugu yeyote kwa kua ndugu zake wengi walishauawa kutokana na
vita ndani ya nchi ya ‘RED ZONE’, huku ndugu
engine wakiwa wamekimbia na kuelekea nchi za mbali ambako walihisi kua watakua
salama.
Herera akiwa
maekaa pale pembezoni mwa bahari huku akiwa anavuta kumbukumbu ya maisha
aliyopitia hadi hapo alipofikia kua mtu mziam akiwa amezaliwa kwenye nchi yenye
vita hadi amekua mtu mzima akiwa na watoto wawili lakini bado vita inaendelea,
akakumbuka jinsi alivyobakwa na wanajeshi wa jeshi la kulinda Amani la nchi ya ‘RED
ZONE’kwa kua alikua nib inti mwenye mvuto sana ilitokea wanajeshi wanne
waliokua wamekuja kufanya patro katika kitongoji ch watengwa area, kipindi
hicho herera alikua na umri wa miaka kumi na nane, siku moja akiwa anatoka
kisimani kuchota maji, kisima kilikua umbari wa kilometa mbili kutokana na
uhaba wa maji ulio kikumba kitongoji cha ‘watengwa area’.
Herera akiwa na rafiki
zake wakitoka kisimani kuchota maji, walikutana na wanajeshi nane wa kikosi cha
serikali wakiwa katika doria wale wana jeshi wakawasimamisha kina herera na
rafiki zake wawili kisha mmoja wa wanajeshi akasema, “ Wewe binti mbona mzuri
sana utazani hujazaliwa kwenye vita!”, kisha akamsogelea herera akamuuliza kua
anaitwa nani hereara akajibu kwa woga “naitwa herera”. Yule mwanajeshi
akatabasamu kisha akamshusha herera ile ndoo aliyokua kabeba kichwani.
Kisha akamsogeza herera pembeni
akaanza kumshawishi kua wakafanye mapenzi kwenye vichaka vilivyokua pale
pembeni, lakini herera akakataa, yule mwanajeshi akakasirika akamshika herera
mkono kw anguvu kisha akampeleka pale kwa wenzake akasema “aseeeee!mazee eti
hiki kimanzi kinagoma kufanyiwa, sasa ngoja tukifunze adabu”. Wale wanajeshi
wakawatishia herera na wanzake kua wasipokubali kufanya mapenzi watawaua, wale
wanajeshi wakawashika kwa nguvu wakaambia atakaye piga kelele watampiga risasi,
wakapeleka ndani ya vichaka……………..(nini kilitokea?, usikubali kupitwa ingia www.duniamtandaoni.blogspot.com).
HADITHI: NAYAPENDA MAISHA LAKINI MAISHA HAYANIPENDI
Reviewed by Unknown
on
Novemba 21, 2016
Rating:
Post a Comment