Man City wameifunga Barca kwa mara ya kwanza baada ya michezo mitano
Manchester City wamebakisha ushindi katika mechi moja ili waweze kufuzu hatua ya 16 bora ya Champions League baada ya kutoka nyuma na kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Barcelona kunako dimba la Etihad..
Man City walijikuta wakieuhus bao baada ya Lionel Messi kuitumia vizuri nafasi aliyotengenezewa na Neymar.
City walisawazisha wakati Sergi Roberto alipopoteza mpira na kuruhusu Sergio Aguero na Raheem Sterling kupasiana vizuri kabla ya mpira kumkuta Ilkay Gundogan na kufunga kwa urahisi.
Sterling alikosa moja ya nafasi za wazi kabisa kabla ya Kevin De Bruyne kufunga bao la pili lilitokana na mpira wa adhabu ndogo uliopigwa kutoka umbali wa mita 25.
Vijana hao wa Pep Guardiola ambao walikuwa wakicheza kwa kasi kubwa walipata bao la tatu baada ya Agueo kufanya kazi kubwa na mpira kumkuta Gundogan aliyemaliza kazi.
Andre Gomes almanusura aipe Barcelona bao na kufanya matokeo kuwa 2-2 wakati huo lakini mpira wake uligonga mwamba.
City sasa wanashika nafasi ya pili kwenye Kundi C wakiwa na alama saba, pointi mbili nyuma ya Barcelona, na endapo watashinda kwenye mchezo wao dhidi ya Borussia Monchengladbach Novemba 23 basi watakuwa wamekata tiketi ya kufuzu 16 bora moja kwa moja.
Katika michezo yote mitano iliyopita waliyokutana, Manchester City wamepoteza yote mbele ya Barcelona.
Man City wameifunga Barca kwa mara ya kwanza baada ya michezo mitano
Reviewed by Unknown
on
Novemba 02, 2016
Rating:
Post a Comment