Header AD

NIKOHURU BLOG # APPLE , FACEBOOK NA GOOGLE KUANDIKA BARUA YA PAMOJA KWENDA KWA RAIS TRUMP


Makampuni nguli katika masuala ya teknolojia yameamua kuvunja ukimya hivyo wapo ktk mchakato wa kuandika barua ya pamoja kwenda kwa rais mpya wa Marekani.

Uamuzi huu unafuatia baada ya rais Trump mnamo jan 27 kusaini amri kuzuia watu kutoka katika mataifa 7 ya kiislamu kwa kile anachodai ni kwa sababu za kiusalama.
Katika barua hiyo japo kwa uchache, wamesema wanaunga mkono jitihada zake na serikali yake ila cha muhimu ni wafanyakazi wa google, facebook na apple wanaotoka katika mataifa saba ambayo yamewekewa vikwazo.

Wanasema "Mafanikio ya makampuni haya yenye ushindani mkubwa katika biashara hayapatikani kutokana na wafanyakazi wazawa tu bali mafanikio hayo pia yanatokana na wafanyakazi kutoka nje ya Marekani"
Katika barua hiyo ambayo bado ipo katika matayarisho haijaweka wazi mengi kwa umma ila kikubwa ni kwa makampuni hayo kupendekeza wafanyakazi wake kuweza kuingia/kutoka Marekani bila kizuizi chochote katika utekelezaji wa majukumu yao.
Barua hiyo ambayo itakuwa imebeba muhstakhabali wa wafanyakazi ambao si wazawa wa Marekani itawasilishwa kwa Rais TRUMP baada ya kukumilika.

TIMU KAZI YA NIKOHURU BLOG ITAENDELEA KUKUPASHA HABARI KUNTU KATIKA NYANJA MBALIMBALI, HIVYO BASI NAWE MPENZI MSOMAJI WA BLOG YETU USISAHAU KUTU"FOLLOW INSTAGRAM , TWITTER na KU'LIKE PAGE YETU FACEBOOK
NIKOHURU BLOG # APPLE , FACEBOOK NA GOOGLE KUANDIKA BARUA YA PAMOJA KWENDA KWA RAIS TRUMP NIKOHURU BLOG # APPLE , FACEBOOK NA GOOGLE KUANDIKA BARUA YA PAMOJA KWENDA KWA RAIS TRUMP Reviewed by Unknown on Februari 07, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads