Header AD

NAYAPENDA MAISHA LAKINI MAISHA HAYANIPENDI



STORY: NAYAPENDA MAISHA LAKINI MAISHA HAYANIPENDI
SEHEMU YA (1)
MWANDISHI: ZABRANCO.
                                                0757035284


 Herera akiwa anatafakari juu ya wapi atapata chakula cha kuwapa watoto wake waliokua wamekumbwa na janga la njaa kubwa kutokana na vita iliyotokea katika nchi ya RED ZONE
. Watu wengi mamia kwa maelfu walikua wakipoteza uhai kwa matatizo mbalili mbali huku wengi wao wakiwa wanakufa kutokana na mabomu yaliyokua yakipigwa na wapiganaji walio kua wakipigana katika nchi ya RED ZONE. Herera akiwa bado kakaa kando kando ya bahari huku akiwa anawaza na kuwazua ni kivipi ataweza kukimbia kutoka nje ya nchi ya RED ZONE, akawa anasikia milio ya risasi ikizidi kulindima upande wa kitongoji cha watengwa area, roho ikazidi kumuuma kwa machungu aliyokua nayo kila alipokua anakumbuka ndugu zake waliokufa vifo vibaya kwa kupigwa mabomu pamoja na risasi kutioka kwa wapiganaji wa kikundi cha WORLD TERRORS. Herera akaumbuka jinsi baba na mama yake walivyouawa kikatili kipindi alipokua mdogo akiwa na umri wa miaka sita, akakumbuka siku ambapo wapiganaji wa world terrors walipovamia kitongoji chao cha WATENGWA AREA walianza kupita nyumba hadi nyumba wakiwalazimisha watu kujiunga katika kikundi chao, ndipo baba na mama wa herera walipokataa kujiunga na hilo kundi, yule mkuu wa kile kikundi aliyekua kavalia sare za kijeshi akawasogelea wote wawili, kisha akatoa kisu akamkata sikio baba yake herera, msichana herera alipoona kua baba yake anatendewa unyama kama ule, akamsogelea yule mkuu wa kile kikundi kisha akamrukia mguuni akamng’ata mkuuni huku akiwa kakaza jino lake kwenye mguu wa wa yule katili, ghafrla yule mkuu akarusha teke kwa kasi akampiga herera maeneo ya ubavuni, herera akaruka hadi upande wa pili kwa jinsi lile teke lilivyokua ana kasi ya ajabu, herera akapiga kelele huku akiwa anashika eneo la ubavu wake kuashiria kua ameumia sana. M ama wa herera alipoona mwanae anafanyiwa ukatili wa kinyama kama ule akataka kwenda kumsaidia mwanae lakini alipotaka tu kikimbila palel alipoangukia mwanae ghafla mmoja wa wapiganaji wa lile kundi akampiga risasi ya mguu.






                            Mama wa herera akaanguka chini huku akipiga mayowe kwa maumivu makali aliyokua akiyapata , yule mpiganaji akamsogelea mama wa herera kisha akatoa kisu kikubwa kilichokua kinaghaa kama almasi iliyopakwa mafuta ya ukatili, kisha akataka kumchinja mama wa herera lakini herera akasema kwa kilugha chao “nooooooooo! Usiue mama yanguu njooo ua mimi” kwa kua herera alikua bado nib inti mdogo sana akiwa na miaka sita tu, yule mpiganaji akacheka kwa dharau kisha akaweka kile kisu shingoni kwa mama wa herera ghafla baba wa herera akajitutumua akawaacha wale wapiganaji akamrukia yule aliyekua anataka kumchinja mke wake, lakini kwa bahati mbaya yule mpiganaji akawa kisha muona baba wa herera alipotaka tu kumkaba yule mpiganaji kwa jina la ‘umuntu’, akamchoma kisu cha tumbo baba wa herera kisha akakizungusha kwa nguvu utumbo ukamwagika chini huku damu ikiwa imetapakaa pale ghafla…………………..(itaendelea usikose mkasa huu, share blog hii kwa marafiki zako WWW.DUNIAMTANDAONI.BLOSPOT.COM).
NAYAPENDA MAISHA LAKINI MAISHA HAYANIPENDI NAYAPENDA MAISHA LAKINI MAISHA HAYANIPENDI Reviewed by Unknown on Novemba 20, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads