Header AD

Ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya soka ya Brazil imeanguka

Ndege iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense kutoka Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji wa Medellin nchini Colombia, mamlaka zathibitisha.



Taarifa kutoka eneo la tukio bado hazijakamilika ila zipo zinazosema kuwa kuna watu waliopona.

Maofisa wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Copa Sudemericana dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.

Kutokana na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.

Ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya soka ya Brazil imeanguka Ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya soka ya Brazil imeanguka Reviewed by Unknown on Novemba 29, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads