NIKOHURUBLOG#Hawa ndiyo wamiliki wa mitandao ya kijamii mikubwa duniani
miongoni mwa vitu vinavyoweza kuibadili dunia ni mitandao ya kijamii haswa Faceebook Twitter, Instagram pamoja na Snapchat. Kila mmoja anaitumia vile awezavyo na hapa sasa tuone watu wanaomiliki mitandao hiyo na utajiri wao .
mtandao Instagram ndio unatoa hela ndefu katika watu wengi kupata matangazo watu ambao waliokuwa na wafuasi wengi yaani ‘Followers’ wanapiga pesa sana japo mitandao mingine pia inapiga pesa .
1.KEVIN SYSTROM
Huyu ndiye mmiliki halali wa mtandao wa Instagram ambapo aliizindua Oktoba 6 mwaka 2010, na moja ya sheria za mtandao huu hauruhusiwi kuufungua ukiwa chini ya miaka 17 hivyo kama unataka kufungua ukurasa huu lazima uwe na umri kuanzia miaka 18. Kevin ana utajiri wa wa dola za kimarekani 1.1 Bilioni.
2.MARK ZUCKERBERG
Wale watu wa mtandao wa Facebook ambao umetupa jeuri sana na ndio mtandao namba moja uliowateka wengi na bado unawateka wengi haswa kwa aina yake ya uungwaji wa picha na vitu mbalimbali vinavyopatikana humo. Wakati inatoka tulifurahi sana mimi nimejiunga na mtandao huu mwaka 2009 sasa utaweza kujiuliza mtandao huu uliundwa mwaka gani ? Facebook imeanzishwa February 4 mwaka 2004 na huyu ndiye mwenye pesa ndefu sana miongoni mwa wamiliki wa mitandao hii ana utajiri wa dola za Marekani 55.3 Bilioni.
3.JACK DORSE
Huyu naye ndio mmiliki wa mtandao wa Twiter mkazi wa Marekani , huu unaaminika kuwa mtandao unaowakilisha watu wanaojielewa haswa wengi wanatumia mtandao huu ku-Tweet na kupashana habari mbalimbali jamaa anamiliki mtonyo wa Dola za Marekani 1.2 Bilioni hadi kufukia mwezi wa nane mwaka huu.
wapo na wanaomiliki mitandao mingine kama Imo Skypepamoja na Snapchat basi kaa nasi ili ujue mengi yanaendelea duniani. Ila kwa ufupi hii ndio mitandao inayofanya vizuri sana duniani
NIKOHURUBLOG#Hawa ndiyo wamiliki wa mitandao ya kijamii mikubwa duniani
Reviewed by Unknown
on
Novemba 22, 2016
Rating:
Post a Comment