Header AD

Ukweli wa ile sayari ya NIBIRU au PLANET X ambayo inaielekea kugonga dunia kwa kasi ya ajabu

Ile Sayari ya Nibiru au Planet X ambayo wanasayansi duniani wamedai inaielekea dunia kwa kasi ya ajabu na huenda ikaipiga, habari mpya ni kwamba imekaribia lakini pia tukio la kupatwa kwa jua, Septemba Mosi, mwaka huu inazidi kuwapa hofu
wanasayansi hao kuwa dunia imefikia ukingoni,
Kwa mujibu wa taarifa za kisayansi, sayari hiyo iliyogunduliwa mwaka 1982 na Taasisi ya Anga za Juu ya Marekani (Nasa) ikiwa nyuma ya Sayari ya Pluto ambayo ni ya mwisho, inakimbia kwa kasi ya maili 200 kwa sekunde.
MAKADIRIO YA WANASAYANSIKatika taarifa yao ya hivi karibuni, wanasayansi wa nchi za Ulaya walisema Nibiru ingeipiga dunia Machi 2015, 2016 au 2017 ambapo mpaka sasa wanaendelea na uchunguzi zaidi.
MWELEKEO WAKEWaliongeza kuwa tangu kuonekana kwake mwaka 1982, sayari hiyo inayowakunisha vichwa wanasayansi duniani, imeshika mwelekeo wa moja kwa moja kuifuata dunia bila kwenda kulia au kushoto hivyo kuwa na wasiwasi kwamba itaigonga dunia na kusababisha mlipuko mkubwa.
IMEANZA KUONEKANA DUNIANI
Awali, sayari hiyo ilikuwa ikionekana na vifaa maalum kama vile satelaiti lakini kwa sasa inadaiwa kuwa baadhi ya nchi kama Canada, Marekani hasa maeneo ya Alaska na baadhi ya nchi za Ulaya hususan za Scandnavia zimeanza kuiona sayari hiyo kwa karibu wakati jua linapochomoza asubuhi na kuwa kama ‘majua’ mawili.
HAKUNA KIZAZI KINGINEKatika kuitafiti sayari hiyo, wanasayansi wamegundua kuwa huingilia mzunguko wa jua (solar system) kila baada ya miaka 3600, jambo linaloonesha wazi kwamba baada ya kutokea safari hii, hakuna kizazi kilicho hai sasa kitakachoshuhudia tena tukio hilo.
TUKIO LA AJABU KUONEKANA ANGANITafiti za wataalam hao zinasema kuwa, itakapokuwa kwenye anga la dunia, sayari hiyo itaonekana mfano wa mwezi hivyo wanadamu kuona angani kuna miezi miwili yenye ming’ao sawa, jambo ambalo litashangaza wengi.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI NA DUNIAMatetemeko ya ardhi, vimbunga, milipuko ya volcano na tsunami vinaelezwa kuwa ni dalili ya kwamba sayari hiyo imeingia kwenye mzunguko wa dunia.
KAMA HAITAGONGA DUNIAUchambuzi zaidi unasema kuwa Endapo kama Nibiru haitaigonga dunia moja kwa moja, basi itatumia muda wa wiki 7 au siku kama 51 kupita kwenye anga la dunia na kutokomea zake huku ikisemekana kwamba, wanasayansi wa mashirika makubwa kama NASA watatangaza kwenye vyombo vya habari itakapofika kabisa ambapo karibu watu wote duniani wataiona.
WACHUNGAJI WAUNGANISHA NA KITABU CHA MUNGUBaadhi ya watumishi wa Mungu, wameingiza ujio wa Nibiru kuwa umeandikwa katika Biblia, Kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Sura ya 8: 10-11, usemao; Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, ilikuwa ikiwaka kama taa. Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga.
Theluthi ya maji ikawa pakanga na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.
Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa na theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake wala usiku vivyohivyo.
MATAMKO YA VIONGOZI WA DINIViongozi mbalimbali wa dini waliopatikana kwa simu au kwa kutumia maneno ya nyuma kwenye mahubiri yao wanadhihirisha kama ifuatavyo….
ALHADJI MUSSA SALIM; Yeye ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema:
“Hizo zote ni dalili kubwa kwa Mungu kututaka wanadamu tujue Mungu yupo maana tumemsahau sana. Hapo hakuna kutishana, watu wamrudie Mungu, adhabu yaja.”
POLYCARP KADINALI PENGOYeye ni Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Katika mahubiri yake amekuwa akisisitiza wanadamu kumrudia Mungu kwa vile wakati wa hukumu umekaribia japokuwa haijulikani siku wala saa.
ZACHARY KAKOBEAskofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel & Bible Fellowship, yeye alisema: “Mwisho wa dunia umekaribia. Hakuna kukwepa wala kupakana mafuta, wanadamu watubu sasa kwa kuwa saa ya hukumu imefika. Hayo yote ni dalili tosha.”
MAALIM HASSAN YAHAYA HUSSEINNi mnajimu na mtabiri mkubwa nchini, yeye anasema: “Kwanza kupatwa kwa jua au mwezi kwa siku hizi ni mara kwa mara tofauti na zamani. Hii ni ishara ya ujio wa maangamizi makubwa duniani.”
KUPATWA KWA JUA, SEPTEMBA MOSI
Kwa upande wa kupatwa kwa jua, Septemba Mosi, mwaka jana, kulikosemwa na kifaa cha kisayansi NASA kinachosafiri nje ya dunia kupitia sayari zote, wanasayansi walisema ni kitendo cha ajabu sana kwani nchi zilizoona tukio hilo, sababu nyingine ilkua ni asubuhi ya saa moja, na nyingine ilikua mchana jambo ambalo ni nadra kwani mara nyingi jua hupatwa mchana ama alasiri na kuelekea jioni.
Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya pamoja na kijiji cha wanging’ombe mkoani njombe ndiyo palikua na giza totoro siku hiyo kwa dakika 3 na takriban sekunde 6 za mnato hivyo kuingia kwenye historia ya dunia.

Ukweli wa ile sayari ya NIBIRU au PLANET X ambayo inaielekea kugonga dunia kwa kasi ya ajabu Ukweli wa ile sayari ya NIBIRU au PLANET X ambayo inaielekea kugonga dunia kwa kasi ya ajabu Reviewed by Unknown on Januari 15, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads