Mwalimu aliyepewa mimba na Mwanafunzi wake afungwa Jela miaka 10
Mwalimu mmoja wa Shule ya elimu ya kati ya Houston, Marekani, Alexandria Vera (24) amehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kutoka kimapenzi na mwanafunzi wake hali iliyopelekea mwalimu huyo kupata mimba.
Akitoa hukumu kwa mwalimu huyo, Hakimu wa Mahakama ya Houston, Michael McSpadden alisema hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa walimu wengine kwani wanataka walimu wawafundishe wanafunzi na sio kufanya mambo mengine.
“Tunataka wanaotoa elimu wawafundishe wanafunzi wetu, tunahitaji mikono yao iwe mbali na wanafunzi,” alisema McSpadden.
Aidha McSpadden alisema alitaa kumpa adhabu ya miaka 30 gerezani lakini aliamua kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa na mimba ya mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akimfundisha shuleni na kuishi nyuumba moja.
Awali Alexandria Vera alisema kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na mwanafunzi huyo mwaka 2015 wakati alipokuwa darasa la nane na baada ya hapo walianza kuishi pamoja lakini kwa ruhusa ya wazazi wa mwanafunzi.
Alisema wazazi wa mwanafunzi huyo walikubali wawili hao kuishi nyumba moja ili awe anamfundisha lakini walianza kuwa wakishiriki tendo la ndoa karibu kila siku jambo lililosababisha mwalimu kupata mimba.
Nae mmoja wa wanafunzi wa shule ambayo mwalimu huyo alikuwa akifundisha alisema kuwa amewahi kushuhudia mwanafunzi mwenzake akimshika mwalimu makalio mbele ya darasa bila mwalimu kuchukua hatua yoyote.
Mwalimu aliyepewa mimba na Mwanafunzi wake afungwa Jela miaka 10
Reviewed by Unknown
on
Januari 15, 2017
Rating:
Post a Comment