Header AD

Video-Ushindi wa Arsenal umevunja rekodi ya miaka 7 Champions League


Mesut Ozil usiku wa kuamkia leo ameifungia Arsenal goli bora na muhimu baada ya timu yake kutoka kuwa nyuma kwa magoli 2-0 mpaka kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ludogorets Razgrad na kufanikiwa kutinga moja kwa moja hatua ya 16 ya Champions League.
Ozil alifunga goli hilo baada ya kumpiga kipa kanzu ya kiaina na kuwapiga chenga mabeki wawili wa Ludogorets kabl ya kufunga kiulaini sana goli hilo na kuipa timu yake ushindi wa dakika za mwisho.
Mapema wakati mpira unaanza, matumaini makubwa ya Arsenal yalikuwa ni kurudia ushindi wao wa magoli 6-0, lakini walijikuta wakipigwa magoli mawili ya haraka kupitia kwa Jonathan Cafu na Claudiu Keseru.
Granit Xhaka aliifungia Arsenal goli la kwanza kutoka umbali wa mita 15 kufuatia krosi nzuri ya Mesut Ozil kabla ya Olivier Giroud kufunga goli la pili kwa kichwa kufuatia kazi nzuri ya Aaron Ramsey.
Kipa wa Arsenal David Ospina aliokoa hatari mbili kwenye lango zilizosababishwa na Wanderson kabla ya Ozil kuzima ndoto za Ludogorets na kufuzu moja kwa moja 16 bora na kuendeleza rekodi yao ya kucheza mechi 15 bila kupoteza.
Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda mchezo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu September 2009 (Pia walishinda 3-2 dhidi ya Standard Liege).

Video-Ushindi wa Arsenal umevunja rekodi ya miaka 7 Champions League Video-Ushindi wa Arsenal umevunja rekodi ya miaka 7 Champions League Reviewed by Unknown on Novemba 02, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads