Header AD

Hii inawahusu waliowahi kutoa mimba ,fanya haya... itakusaidia .

Jamii yetu imekumbwa sana na janga hili la utoaji wa mimba hasa kwa mabinti wadogo ambao wengi wao wapo vyuoni na mashuleni.
Na Kwa vile kulikuwa na maswali mengi niliyoulizwa nini cha kufanya kwa ambao tayari wameshatoa mimba sasa ungana name ili tujuzane. 
Mambo yenyewe ni haya…
ONANA NA MTAALAMU WA USHAURI:
Kama  una mawazo mengi kwanini umetoa mimba na unajutia maamuzi yako au moyoni unahisi umefanya kosa kubwa kwa binadamu au mungu wako nenda unana na mshauri na atakusaidia kurudi katika hali yako ya kawaida.
NENDA HOSPITALI UONANE NA DAKTARI;  
Ukitoa  mimba kuna madhara mengi yanayofuatia ikiwemo ugumba, na kuharibika viungo vya uzazi.. nenda ukapige picha ya ultrasoundkuangalia hali ya viungo vya uzazi, na kama vinaumwa vianze kutibiwa mapema iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika. Pia pima magonjwa mengine ya kuambukizwa ikiwemo ukimwi, kaswende na gono kwani ni magonjwa yanayo ambatana na ngono zembe. usiogope hakuna daktari wa kukupeleka polisi kwa kutoa mimba..
CHAGUA NJIA YA UZAZI WA MPANGO
Kuna  watu wameshatoa mimba mpaka tano sasa hivi, mimi naona huo ni uzembe kwani kuna njia nyingi sana za kuzuia ujauzito. Kama huwezi kondomu njia ya kijiti ni nzuri kuliko zote kwani siku ukitaka mtoto unakitoa kijiti na kunasa mimba haraka. njia ya kalenda ni nzuri pia ila wengi hawaiwezi na inataka umakini sana hivyo achana nayo..Acha kusikiliza kelele za watu eti njia hizo zina madhara kwani hizo ni imani potofu na ukipuuzia utaendelea kutoa mimba zaidi kitu ambacho ni hatari kiafya.
TUMIA VIRUTUBISHO VYA UZAZI;

Mara nyingi kutoa mimba huharibu mfumo wa homoni za uzazi wa wanawake na  maumbile ya uzazi. Hali  hii ni hatari na ndio hufanya wanawake wengi kushindwa kubeba mimba siku za usoni. Tumia  virutubisho vya multmaca ambavyo vimesaidia sana kurudisha hali ya homoni katika kawaida yake na kusaidia kubeba mimba kwa wanaozitafuta.
Hii inawahusu waliowahi kutoa mimba ,fanya haya... itakusaidia . Hii inawahusu waliowahi kutoa mimba ,fanya haya... itakusaidia . Reviewed by Unknown on Desemba 26, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads