Donald Trump: Nitashirikiana na Urusi na China
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kushirikiana na Urusi na China, iwapo mataifa hayo yatashirikiana naye.
Katika mahojiano na Wall street journal, bw Trump amesema vikwazo vilivyowekewa Urusi hivi majuzi, vitaendelea kuwepo, japo huenda vikaondolewa iwapo Urusi itasaidia Marekani katika vita dhidi ya ugaidi.
Anatumai kwamba atakuwa na kikao na rais Putin hivi karibuni.
Pia amesema kuwa sera ya One China ambayo Marekani haitambui Taiwan itajadiliwa upya.
Wakati huohuo kamati ya bunge la seneti nchini Marekani imetangaza kwamba itachunguza madai kwamba urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.
SOURCE:BBC News
Donald Trump: Nitashirikiana na Urusi na China
Reviewed by Unknown
on
Januari 15, 2017
Rating:
Post a Comment