Marekani yakubali kuiuzia Kenya ndege za kivita
Marekani imekubali kuiuzia serikali ya Kenya ndege za kivita na vifaa vingine vya kijeshi, kwa kima cha Dola Milioni 418 sawa na Shilingi za Kenya Bilioni 43.5.
Tayari bunge la Congress limepitisha kufanyika kwa manunuzi hayo na kutoa leseni ya kuidhinisha hilo.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Kenya itapokea ndege hizo aina za AT-802L na AT-504 na vifaa vingine vya kivita.
Marekani inasema ni muhimu sana kwa Kenya kupata vifaa hivyo kwa sababu ni mshirika muhimu na wa karibu sana katika vita dhidi ya kupambana na ugaidi hasa kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia.
Kenya inatarajiwa kutumia silaha hizi kuendelea kupambana na kundi la Al Shabab nchini Somalia ambalo limeendelea kutishia kuishambulia nchi hiyo kwa kujiunga na wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM mwaka 2011.
Wiki iliyopita, rais mpya wa Marekani Donald Trump alihoji umuhimu wa nchi yake kuendelea kuunga mkono vita dhidi ya Al Shabab nchini Somalia, baada ya kutofanikiwa kwa miaka 10 sasa.
Credit: RFI
Credit: RFI
Marekani yakubali kuiuzia Kenya ndege za kivita
Reviewed by Unknown
on
Januari 25, 2017
Rating:
Post a Comment