Header AD

Nay wa Mitego Amlilia Mwanamke Aliyedhalilishwa kwa kuchapwa Viboko

Rapa Nay wa Mitego ameonesha kusikitishwa na moja ya video ambayo inamuonesha mwanamke akiwa amezungukwa na wazee na vijana wengi wakimchapa viboko kama adhabu kutokana na makosa ambayo mwanamke huyo ameyafanya.

Rapa Nay wa Mitego baada ya kuitazama video hiyo amefunguka na kusema licha ya ubabe wake na ukorofi wake lakini katika maisha yake hajawahi kumpiga mwanamke na kusema anawachukia sana wanaume ambao wamekuwa wakiwapiga wanawake.

"Na ubabe wangu wote, sijawahi kumpiga mwanamke, namchukia mwanaume yoyote kwenye hii dunia anaye mpiga mwanamke. Ningekua ni kiongozi kwenye hii nchi hawa mbw*** wote wangeenda jela bila mjadala, acha jela ikajae lakini cha moto wakione. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu. Sijui kabila gani hawa mashetani..!! eeh Mungu walaani hawa binadamu wanaomdhalilisha huyu mama, wageuze ata funza tu. Wahusikaaaaa please chukue hatua kali juu hili". Alisisitiza Nay wa Mitego

Tazama hapa video ya mwanamke huyo, akiadhibiwa na kundi la wanaume...
 

Nay wa Mitego Amlilia Mwanamke Aliyedhalilishwa kwa kuchapwa Viboko Nay wa Mitego Amlilia Mwanamke Aliyedhalilishwa kwa kuchapwa Viboko Reviewed by Unknown on Januari 10, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads