Header AD

NIKOHURUBLOG# Ugonjwa Wa Saratani Ya Ngozi (Melanoma)

WIKI iliyopita tulieleza jinsi ugonjwa huu unavyomuingia mtu na matatizo yake.
Tulieleza dalili lakini nyingine ni tezi za mwili za kwenye makwapa na kwenye nyonga huvimba, mgonjwa atatokwa na uvimbe kwenye ngozi, atapoteza uzito kwa kasi bila kujua sababu, atapata kikohozi kisichoisha, atapoteza fahamu au kupata kifafa,  ataumwa kichwa.
TIBA
Kuna tiba nyingi za kitabibu, zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni dawa na ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa.

Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto ambayo yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini, kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko wa damu, kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.

Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku mtu anywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho au mkojo.

Ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.

Maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kutokana na umuhimu huo ni vyema kunywa maji  ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.

Faida nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo kufanya kazi kikamilifu, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja.

USHAURI
Unashauriwa kunywa maji moto kabla ya kufanya mazoezi kwani huko ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa sumu. Maji ya moto yakifika tumboni yanaanza kufanya kazi moja kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.

Unywaji wa maji ya moto kabla ya mazoezi ni mzuri kwani mtu anakuwa kama amekula chakula. Kunywa maji ya baridi bila kuweka kitu tumboni na kwenda kufanya mazoezi kunaweza kusababisha tumbo kuuma au maji kucheza wakati wa kukimbia kama unafanya mazoezi ya kukimbia.

Maji ni muhimu kwa mwili wako,  yakiwa ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenye rangi ang’avu. Ushauri ni kuwa ukiwa na alama yoyote mwilini inayokua kamuone daktari haraka.
NIKOHURUBLOG# Ugonjwa Wa Saratani Ya Ngozi (Melanoma) NIKOHURUBLOG# Ugonjwa Wa Saratani Ya Ngozi (Melanoma) Reviewed by Unknown on Januari 10, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads