Sare Zatawala Mechi Za Ufunguzi Afcon, Bossou Wa Yanga Kazini Leo
FAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika zimeanza kwa sare za kufanana jana, mechi zote zikimalizika kwa sare ya 1-1 mjini Libreville, Gabon.
Burkina Faso ilitoka nyuma na kupata sare ya 1-1 dhidi ya Cameroon katika mchezo wa Kundi A. Nahodha Benjamin Mounkandjo aliifungia Cameroon bao la kuongoza dakika ya 35 kabla ya Issoufou Dayo kuisawazishia Burkina Faso dakika ya 72.
Katika mchezo wa ufunguzi, wenyeji Gabon walishindwa kulinda bao lao la kuongoza na wakajikuta pia wanamaliza mechi kwa sare ya 1-1.
Bao la dakika za lala salama kabisa la Juary Soares liliipokonya tonge mdomoni Gabon iliyotangulia kwa bao nyota wake, Pierre-Emerick Aubameyang mjini Libreville.
Mapema sherehe za ufunguzi zilipambwa kwa burudani mbalimbali za wasanii kama Diamond Platnumz wa Tanzania na Rapa Mfaransa Booba, kabka ya Rais wa Gabonese, Ali Bongo kwenda kufunguia rasmi mashindano.
Bongo aliongozana na Rais mwenzake wa Guinea-Bissau, Jose Mario Vaz, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CFA), Issa Hayatou.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za Kundi C, maningwa watetezi Ivory Coast wakimenyana na Togo ya beki wa Yanga, Vincent Bossou na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikimenyana na Morocco usiku

Reviewed by Unknown
on
Januari 15, 2017
Rating:
Post a Comment