YAFUATAYO YATATOKEA MWILINI NDANI YA DAKIKA 60 BAADA YA KUNYWA COCACOLA
Watu wengi wameendelea kufurahia kinywaji cha Cocacola japokuwa wanatambua maudhi/matokeo yake ndani ya miili yetu, Listi hapo chini ni vitu vichache utakavyopata/tokea mwilini mwako baada ya wewe kunywa chupa moja tu ya kinywaji cha Cocacola!!
DAKIKA 10 ZA KWANZA
Takribani vijiko 10 vya sukari vinaingia katika mzunguko wako wa damu mwilini, sukari hiyo hutaitapika ili itoke! La hasha Phosphorus acid iliyopo mwilini itasaidia kupunguza uwingi huo, hivyo utajisikia uzuri kabisa.
BAADA YA DAKIKA 20
Kiwango chako cha sukari katika damu hupanda, hali hii hupelekea INSULIN kumwagwa kwa wingi kupunguza sukari hii katika damu, Ini nalo huhusika kubadili hii sukari iwe katika mfumo wa GLYCOGEN!!
BAADA YA DAKIKA 40
Wakati huu CAFFEIN iliyomo katika Cocacola hufyonzwa yote na kuingia mwilini!. Pupili(Ni ogani inayoratibu mwanga unaoingia katika jicho)za macho hutanuka, Presha ya damu hupanda,Hii hupelekea Ini kumwaga sukari nyingi katika damu.Vipokezi vya Adenosine kwenye ubongo hufungwa kuzuia binadamu kuishiwa nguvu/kupata kizunguzungu.
DAKIKA YA 45
kiwango cha homoni ya dopamine hupanda, vipokeo vya dopamine katika ubongo hunasa homoni hii na kupelekea muhemuko/Ashiki ya mwili kuwa juu. Basi Cocacola itakuwa imefanya kazi sawa kabisa na madawa ya kulevya aina ya Heroine!!
DAKIKA YA 60
ulichokuwa umekunywa sasa huisha mwilini, sukari katika damu hushuka ghafla, na utakuwa tayari umekojoa maji yote ulokuwa umekunywa kupitia cocacola yako.laiti kama maji hayo yangetumika mwilini ungalinufaika!!
Phosphoric acid hunyonya kiwango kingi cha madini ya Calsium, Magnesium, na Zinc(Ambayo hutumika pia katika kujenga mifupa imara na kuimarisha meno) katika utumbo mdogo, hali hii huongeza kasi ya umeng'enyaji wa chakula hivyo utahisi njaa mapema. hii huenda sambamba na uwingi wa sukari na viongeza ladha vya Cocacola hivyo utakojoa kiwango kikubwa cha Calsium!!. Pia uwepo wa Caffeine hupeleke upoteze kiwango kingi cha Calsium, magnesium, Zinc na maji mwilini!!
ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YETU NIKOHURU BLOG uweze kupata makala kuntu za masuala mbalimbali!!
YAFUATAYO YATATOKEA MWILINI NDANI YA DAKIKA 60 BAADA YA KUNYWA COCACOLA
Reviewed by Unknown
on
Januari 10, 2017
Rating:
Post a Comment