Mahakama kuu ya China: Trump ni adui wa utawala wa sheria duniani
Mahakama Kuu ya China imemtaja Rais Donald Trump wa Marekani kuwa adui wa utawala wa sheria duniani.
Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo kupitia jaji mkuu wa nchi hiyo imesema kuwa, misimamo inayotolewa na rais huyo ambayo imesababisha changamoto nchini Marekani,
imekuwa chanzo cha kuibuka uadui dhidi ya sheria. Aidha imeongeza kuwa, misimamo ya rais huyo imeinyima mahakama ya Marekani uhuru wake katika maamuzi.
Hii ni katika hali ambayo Wizara ya Sheria nchini Marekani inajaribu kuchunguza hukumu zilizotolewa na mahakama tisa za nchi hiyo katika kupinga misimamo ya Rais Trump. Mahakama hizo zimesisitiza kuwa, rais huyo hana haki ya kuwazuia raia Waislamu kuingia Marekani na hivyo viwanja vyote vya ndege na mipaka ya nchi hiyo vinatakiwa kufunguliwa kwa ajili ya kuingia watu hao.
Siku chache zilizopita pia, Joe Chiang, Mkuu wa Mahakama Kuu ya Watu wa China aliwataka majaji wa nchi yake kutupilia mbali mienendo isiyo sahihi ya Wamagharibi sambamba na kuwataka wasiruhusu kuingiliwa kisiasa uhuru wa vyombo vya mahakama nchini humo
SOURCE: ParsTODAY
Mahakama kuu ya China: Trump ni adui wa utawala wa sheria duniani
Reviewed by Unknown
on
Februari 09, 2017
Rating:
Post a Comment