NIKOHURU BLOG# Chelsea Kileleni Mwa Ligi kwa Pointi Tisa
Chelsea ililazimika kutoka sare dhidi ya timu ya Liverpool ilioimarika katika uwanja wa Anfield baada ya penalti ya Diego Costa kupanguliwa na kipa Simon Mignolet lakini bado
wakaongeza uongozi wao katika kilele cha ligi ya Uingereza na pointi tisa.
Kipa wa Liverpool Mignolet alirekebisha makosa yake baada ya kupatikana amezubaa na mkwaju wa adhabu wa David Luiz.
Kichwa cha karibu cha Georginio Wijnaldum kunako dakika ya 11 baada ya muda wa mapumziko kiliipatia Liverpool sare waliohitaji, na hivyobasi kusitisha msururu wa matokeo mabaya ambao ulikuwa umekumba timu hiyo.
Matokeo hayo yalisababisha kubanduliwa kwa timu hiyo katika kombe la EFL pamoja na lile la FA.
Hatahivyo ingekuwa bora zaidi kwa Chelsea na vibaya zaidi kwa Liverpool baada ya Costa kuangushwa na Joel Matip dakika 14 kabla ya kukamilika kwa mtanange huo.
Refa Mark Clattenburg alitoa penalti kwa upande wa Chelsea lakini kipa Mignolet akaokoa penalti hiyo
NIKOHURU BLOG# Chelsea Kileleni Mwa Ligi kwa Pointi Tisa
Reviewed by Unknown
on
Februari 02, 2017
Rating:
Post a Comment