AFCON 2017: HATIMAE MISRI WATINGA FAINALI
Mabingwa wa kihistoria barani Afrika, timu ya taifa ya Misri wametinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya AFCON inayoendelea nchini Gabon.
Misri wamefanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo, baada ya kuiondoa Burkina Faso kwa mikwaju ya penati nne kwa tatu, ambayo ililazimika kupigwa kutokana na wawili hao kwenda sare ya bao moja kwa moja katika dakika 120.
Katika dakika ya 66 Misri walipata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wao anaecheza soka nchini Italia kwenye klabu ya AS Roma Mohamed Salah, lakini dakiika saba baadae Aristide Bance aliisawazishia Burkina Faso.
Katika mikwaju ya penati mchezaji mwenye umri mkubwa katika fainali za Afrika za mwaka huu, mlinda mlango Essam El Hadary aliibuka shujaa baada ya kupangua mikwaju miwili ya Burkina Faso na kuiwezesha Misri kutinga katika mchezo wa fainali.
Hii ni mara ya nane kwa timu ya taifa ya Misri kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya Afrika, tangu ilipoanzishwa mwaka 1957.
Timu hiyo imetwaa ubingwa wa Afrika mara saba na kumaliza katika nafasi ya pili mara moja.
AFCON 2017: HATIMAE MISRI WATINGA FAINALI
Reviewed by Unknown
on
Februari 02, 2017
Rating:
Post a Comment