NIKOHURU BLOG# Ilimradi tunashinda, benchi kwangu poa tu – John Terry.
John Terry ndiye mchezaji mkongwe aliyebaki Chelsea kwa sasa.Baada ya Ivanovic kuondoka Terry anabaki kama Legend peke yake katika timu hiyo
.Lakini pamoja na ukongwe wake John Terry kwa sasa hana namba katika kikosi cha Antonio Conte.
Hali ni tofauti kichwani mwa Terry kwani yeye haoni shida haswa kama hachezi huku timu inashinda.Japokuwa Terry amekuwa akiwekwa benchi mara nyingi na Conte lakini chini ya ulinzi wa Cahill na David Luiz Chelsea wameonekana kuimarika sana katika eneo lao la ulinzi na kuongoza ligi hadi sasa.
John Terry amesema kwake yeye kama kutocheza kwake kunaifanya timu ishinde,baasi hayuko tayari kuichezea Chelsea ilimradi siku ya mwisho wabebe kombe.”Naamini kama kutocheza kwangu hakuiletei shida timu na inaendelea kushinda baasi ni bora kubaki hivi hivi,nachukua sana mazoezi na nafurahi na hali ya sasa ya timu,najituma bado kwa kuwa timu ninaipenda na inanijali sana.” alisema Terry.
Toka katika mechi ya Chelsea dhid ya Swansea mwezi wa tisa mwaka jana baada ya hapo hadi leo hii Terry ameichezea Chelsea kwa dakika 6 tu.Mfumo wa 3-5-2 aliokuja nao kocha Antonio Conte unaonekana sii rafiki kabisa kwa Terry lakini Terry anasema Conte amekuwa muwazi sana kwake mara zote.
“Ninafanya sana mazoezi kwa sasa,Conte amenijenga sana kwani mara nyingi huwa tunakimbia na kuifanya timu iwe fiti” alimalizia Terry.Chelsea wamejichimbia kileleni mwa ligi na inaonekana ni ngumu kung’oka,Terry anafurahia maendeleo ya timu yake hata kama akae benchi kila siku ila yete furaha yake ni Chelsea kushinda.
NIKOHURU BLOG# Ilimradi tunashinda, benchi kwangu poa tu – John Terry.
Reviewed by Unknown
on
Februari 03, 2017
Rating:
Post a Comment