Header AD

NIKOHURU BLOG# Rio Fernandi amchana Pogba baada ya ku-post video akicheza ngoma ya Wizkid

Paul Pogba tangu amekuja Man United amekuwa akizungumziwa katika mambo mengi sana.Pogba wakati anakuja United gumzo lilikiwa kuhusu ada yake ya usajili baadae kiwango chake uwanjani kikawa ndio gumzo.Nje ya
uwanja pia Pogna amekuwa akizungumziwa kuhusu maisha yake kwa ujumla.
Kati ya vitu ambavyo Paul Pogba anaonekana kuvihusudu sana ni kucheza muziki.Mara nyingi akifunga goli huwa anashangilia kwa kucheza style ya “Dab Dance”.Huu umekuwa utaratibu wake toka yuko Juventus na hadi sasa United bado Pogba ana “dab” na kucheza mziki kama kawaida.

Sasa baada ya kurudi Manchester United Pogba amekutana na swahiba wake wa kitambo Jesse Lingard.Kama ilivyo kwa Pogba Lingard naye anapenda sana kucheza cheza muziki huku nae “Dab” ikiwa style yake ya ushangiliaji
.
Wiki hii kumetrend video inayomuonesha Pogba na swahiba wake Lingard wakicheza katika vyumba vya kubadilishia nguo.Pogba na Lingard walikuwa wakicheza wimbo wa Wiz Kid uitwao Closer,katika video hiyo pia alionekana kinda wa United Fosouh Mensah.

Video hiyo inaonekana kumkera sana mchezaji mkongwe wa zamani wa timu hiyo Rio Ferdinand.Rio anaona ni ujinga kwa Pogba na Lingard kudance katika wakati huu ambao United wako nafasi ya 6 katika ligi huku leo wakiwa wanajiandaa kuwakabili Hull City.

“Sio kitu sahihi kwa wakati huu,unachezaje wakati timu yako haipo Champions league na haipo karibu na ubingwa?kama wangecheza wakati timu ina kombe la ligi hapo sawa” alisema Rio.Ferdinand alishawahi kuwasema wachezaji wa Arsenal kwa utoto kama huu na anaona ni bora awaambie na wa Manchester United.

Wakati Pogba anapost video hiyo,United hawana uhakika wa kucheza hata Chapions League msimu ujao kwani wako nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi.
NIKOHURU BLOG# Rio Fernandi amchana Pogba baada ya ku-post video akicheza ngoma ya Wizkid NIKOHURU BLOG# Rio Fernandi amchana Pogba baada ya ku-post video akicheza ngoma ya Wizkid Reviewed by Unknown on Februari 02, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads