Russia yasema itapiga kura ya veto dhidi ya muswada wa Baraza la Usalama kuhusu Syria
Russia imetangaza kuwa, itatumia kura ya veto kupinga vikwazo vya aina yoyote ile vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Syria kwa madai kwamba nchi hiyo imetumia silaha za kemikali.
Uamuzi huo wa Russia umetangazwa baada ya kuwepo bahari kwamba baraza hilo linapanga kupasishwa azimio la kuiwekea viwazo serikari ya Syria kwa madai ya kutumia silaha za kemikali.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mashinikizo ya Marekani na waitifaki wake, limekuwa likifanya jitihada za kuibambikizia Syria tuhuma ya kutumia silaha za kemikali licha ya kwamba ushahidi unaonesha kuwa silaha hizo zilitumiwa na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani na washirika wake.
Awali kituo cha utafiti cha IHS cha Marekani kilitangaza kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wametumia silaha za kemikali mara zaidi ya 71 katika nchi za Syria na Iraq dhidi ya raia wa kawaida. Vilevile ripoti za Wizara ya Ulinzi ya Russia zimethibitisha kuwa, kundi hilo la kigaidi limetumia silaha za kemikali mara kadhaa nchini Syria.
Mgogoro wa ndani wa Syria ulianza mwaka 2011 kwa hujuma na mashambulizi makali ya kundi la kigaidi la Daesh ambalo lilianzishwa na kufadhiliwa na Saudi Arabia, Marekani na washirika wao kwa shabaha ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar Assad.
Russia yasema itapiga kura ya veto dhidi ya muswada wa Baraza la Usalama kuhusu Syria
Reviewed by Unknown
on
Februari 25, 2017
Rating:
Post a Comment