Simba Yaitandika Mabao 2 Yanga Uwanja wa Taifa
Klabu ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika za mwanzo kabisa na kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7 mgongoni kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat Lufunga na kupelekea Yanga kupata penati ndani ya ya dakika 4 za mchezo na kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga.
Yanga iliendelea kuongoza kwa bao hilo la kwanza huku wakiwa na moto wa kutafuta goli la pili, katika dakika ya 23 Yanga walipata kona ya kwanza ambayo ilipigwa na mchezaji Haruna Niyonzima lakini kipa wa Simba aliweza kuicheza vyema na kuondoa hatari ya Yanga kupata goli la pili ndani ya dakika za mwanzo mwanzo.
Kocha wa Simba Omug alipoona kikosi chake hakina mwenendo mzuri ndani ya dakika 27 alimtoa Luizio na kumuingiza Said Ndemla ambapo hapo kidogo mchezo kwa upande wa Simba ulibadilika na kuanza kufanya mashambulizi, huku wakijaribu
Ndani ya dakika 32 Goli kipa wa Yanga Deogratius Munishi alidaka mpira na kukaa nao kwa muda na kupeleka faulo ambayo ilipigwa na Said Ndemla wa Simba lakini Ndemla alikosa na kupoteza nafasi ya kusawazisha goli la kwanza.
Yanga iliendelea kufanya vyema na kujaribu mara kadhaa katika lango la Simba bila mafanikio, ndani ya dakika 43 Simba ilibahatika kupata faulo nyingine tena ambayo ilipigwa na mchezaji Ajib lakini mpira huo ulikwenda nje.
Mchezo uliendelea kwa kasi na mashambulio kwa timu zote mbili, na ilipofika dakika ya 47 mchezaji wa Yanga Thabani Kamusoko alitoka nje baada ya kupata majeraha na kuingia Said Juma Makapu.
Mpaka muda wa mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao moja dhidi ya Simba huku ikiwa imetawala mchezo kwa asilimia 51 na Simba ikitawala mchezo kwa asilimia 41.
Baada ya kurudi kwa kipindi cha pili timu zote mbili zilikuwa na hamasa ya mchezo na ushindi hamasa hizo zilipelekea mchezaji wa Yanga, Endrew Vicenti alipata kadi ya njano ndani ya dakika 56 mchezaji wa Simba alipigwa kadi nyekundu na kutoka nje ya uwanja na kuwaacha Simba wakiwa pungufu uwanjani.
Katika kipindi cha pili baada ya kuingia mchezaji Kichuya Simba ilibadilika na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kuonyesha uwezo katika kucheza mpira jambo lililopelekea mchezaji Mavugo wa Simba ndani ya dakika 66 kupata goli la kwanza kwa Simba na kuweza kusawazisha na kuwa bao moja kwa moja.
Mpka dakika ya themanini ya mchezo Simba kupitia kwa mchezaji wake Shiza Ramadhan Kichuya aliiandikia Simba goli la pili dhidi ya Yanga huku timu hiyo ikiwa pungufu uwanjani.
Mpaka mpira umekwisha Simba 2-1 Yanga (Mavugo 66, Kichuya 81 : Msuva 5)
Simba Yaitandika Mabao 2 Yanga Uwanja wa Taifa
Reviewed by Unknown
on
Februari 26, 2017
Rating:
Post a Comment