Header AD

STEVE Nyerere : Naomba radhi kwa viongozi wote niliowataja kwenye mazungumzo yangu na mama sepetu.


Msanii wa Filamu na Muigizaji mahiri hapa nchini Steve Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea hivi karikuni ,likiwe suala la ujumbe wa sauti

ambao umekuwa ukisambazwa katika mitandano ya kijamii ukimuhusisha yeye Steve pamoja na Mama Wema Sepetu.

Katika Mkutano huo STEVE NYERERE amesisitiza kuwa kilichosemwa na WEMA SEPETU kuwa anaidai CCM fedha ni uongo, kwani walilipwa huku akisema Msanii aliyelipwa fedha nyingi katika kazi hiyo ni Wema Sepetu, hivyo anashangaa kusikia akidai kuwa hajalipwa.

Mradi wa Mama Ongea na Mwanao uliratibiwa na Steven Nyerere huku akisaidiwa na Wema Sepetu na kazi yake ilikuwa ni kutoa elimu kwa wazazi kuwa karibu zaidi na vijana wao wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Hata Hivyo, Steve Nyerere, ametumia mkutano huo kukiri kuwa Sauti iliyotumwa kwenye Mitandao ya Kijamii inayohusisha mazungumzo yake na Mama yake Wema Sepetu ni ya kwake, hivyo amewaomba radhi viongozi wote aliowataja katika mazungumzo hayo.

'Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe,"Ile Sauti imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi" ,alisema Steve Nyerere

"Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza,Nimetaja viongozi katika ile sauti halafu mtu anakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya amenikosea sana,Lakini namuachia Mungu"alimaliza kusema
STEVE Nyerere : Naomba radhi kwa viongozi wote niliowataja kwenye mazungumzo yangu na mama sepetu. STEVE Nyerere : Naomba radhi kwa viongozi wote niliowataja kwenye mazungumzo yangu na mama sepetu. Reviewed by Unknown on Februari 26, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads