Header AD

Trump: Iran “inamulikwa” baada ya jaribio la kombora


Rais wa Marekani, Donald Trump

Ujumbe huu umekuja baada ya mlolongo wa Tweets ambazo zilikuwa zikiendelea kulaani mkataba uliofikiwa na Marekani na mataifa mengine matano yenye nguvu katika kuzuia programu ya nyuklia ya Iran
kwa mabadilishano ya kupunguziwa vikwazo walivyowekewa.
Iran tayari imemulikwa rasmi kwa kurusha kombora la masafa marefu. Ilikuwa inatakiwa iwe na shukrani kwa mpango wa kutisha ambao Marekani walikubaliana nao!
Iran ilikuwa mahututi na tayari ikiporomoka mpaka pale Marekani ilipokuja na kuipa tena uhai katika mpango uliowapa dola bilioni 150.
Trump amesema Iran ni lazima iwe na “shukrani” kwa makubaliano hayo, na kuwa nchi hiyo ilikuwa “tayari inaporomoka” kabla ya mabilioni ya dola kurejeshwa mikononi mwao.
Mpango wa nyuklia ulikuja kwa sababu ya shutma za kuwa Iran ilikuwa kwenye hatua za kutengeneza silaha, jambo ambalo Iran ilikanusha, na hivyo Iran ilitakiwa kuweka kikomo katika utengenezaji wa nyuklia na kubadilisha vituo vyake kadhaa vya kinyuklia kwa matumizi mengine.
Iran, Yemen
Jumatano jioni, maafisa wa ikulu ya White House walisema kuwa kitendo cha Iran kurusha kombora la masafa marefu na kusaidia wapinzani wa kihouthi nchini Yemen ni uchokozi, unaleta vurugu katika eneo na kutishia nchi mbalimbali, ikiwemo washirika wa Marekani. Maafisa hao wamesema Marekani itachukua hatua “stahili.”
Alipoulizwa hatua gani Marekani ingechukua, maafisa hao waliishia tu kusema wana idadi kubwa ya hatua hizo. Lakini, wasemaji wa ngazi ya juu wa White House wamesema kurushwa kwa kombora la Iran na uwezekano wa Marekani kuchukua hatua haina mahusiano kabisa na mpango mzima wa nyuklia wa Iran, na White House haijaishutumu Iran kwa kuvunja mapatano ya awali.
Ian Lustick mhadhiri wa sayansi ya kisiasa katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania, ameiambia VOA kuwa Marekani inafaa kuzingatia wakiwa wanataka kukabiliana na Iran katika urushaji wake wa kombora, akitoa mfano kwamba Iran inaweza ikahatarisha maisha ya wanajjeshi 6000 ya Marekani walioko Iraq.
“Wengi wa wananchi wa Iraq ni washia na kwa namna moja au nyengine wana masikitiko makubwa na Iran. Kuna makundi makubwa yenye nguvu ya wapiganaji ndani ya Iraq ambayo yanaongozwa na kupewa mafunzo na wairani. Hivyo ni baadhi ya vikundi vya wapiganaji bora ambavyo vimekuwa na ushindi mkubwa dhidi ya wapiganaji wa Islamic State.
Trump: Iran “inamulikwa” baada ya jaribio la kombora Trump: Iran “inamulikwa” baada ya jaribio la kombora Reviewed by Unknown on Februari 03, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads